1. Jinsi utakavyovalia
Usivalie
kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume
ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja
pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume,
lakini usivuke mipaka ya kawaida.
Kumbuka
kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya
mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue.
2. Unavyomuangalia
Mchungulie
mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa
haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa
kuapproach na anaweza kukupuuza.
3. Mitindo ya kumwangalia
Kuna
mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa
naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka.
i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake
na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole
pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya
kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake.
ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya
kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia,
ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa
confidence na kukuona wewe ukipendeza.
4.Mfanyie kazi iwe rahisi
Inakuwa
vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na
marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa
wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike
mmoja.
5. Sehemu zifaazo
Si
kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume
akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake
kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa,
supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga
stori.
6. Mpatie nafasi aongee na
wewe
Hata
kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe
interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe,
unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio
sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume
huyu kuzungumza na wewe.
7. Tabasamu
Onekana
jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa
kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka
macho ya mwanaume yamwone.
8. Usiboeke
Kuwa
mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua.
Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha
chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na
maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo
na mwanga.
9. Usiwe mjeuri
Kama
wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza
kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna
mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke
ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa.
10. Usitangamane na
wanaume
Hii
ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki
zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi
kamwe.
11. Mwonyeshe kuwa uko
intrested
Mwonyeshe
kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na
marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo
anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako.
12. Onyesha uanawake wako
Mwangalie
mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio
lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama
kugonga ndipo.
13. Mchokore
Pita
mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia,
ataipenda kuona atenshen yake.
14. Usilazimishe
Utakuwa
unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia
mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv