Leo
Naomba niongelee na nitilie mkazo jambo hili, na njia hizi hakikisha
hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana
unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni
kuhusu wanawake.
Hebu
zione hapa njia zote nilizo kuandalia ukizingatia pale unamuonesha isia zako
kwa mara ya kwanza..
Muonyeshe
umempa akili yako na umakini kwa hali flani.
Wanawake
wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa
anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa
mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu
sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa
sifa nyingi katika hali ambayo hazihitajiki
Tengeneza
mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.
Sifa
ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na
mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa
Kutongoza toka moyoni bila hata kufikiria utaongea nini au kujishitukia,
utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na
kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo
atapiga simu na kuanza kujitambulisha, “Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba”, mwenyewe
anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.
Muonyeshe
changamoto.
Mwanamke
akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine
yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja
kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili
kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala,
mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha.
Usimfuatilie
sana.
Usipoonana
na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni
ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako,
iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa
anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubiri
na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia,
utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja.
Muulize
maswali ya namna flani.
Mwanamke
akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika
mkubwa ataendelea kukufikiria kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa
hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia
mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata
fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia gani na
wanaume wa aina hii. Kwahiyo ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya
kifala, patishia huyo mwanamke ataanza kukufikiria kuwa utakuwa na tabia
hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huo ndo utakuwa mwisho
wako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv