Ni mtoto wa nne wa
mmiliki raslimali za majengo jijini New York, Fred Trump. Licha ya
utajiri wa familia yake, alitumainiwa kufanya kazi za daraja la chini zaidi
katika kampuni ya baba yake ambapo alipelekwa kujiunga na jeshi akiwa na umri
wa miaka 13.
Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha
Pennysylvania na akajiweka katika nafasi nzuri ya kurithi utajiri wa baba yake
baada ya kaka yake mkubwa, Fred, kuwa rubani.
Fred Trump alifariki akiwa na umri wa miaka 43
kutokana na ulevi na uvutaji sigara.
Ufanisi wake katika utajiri wa familia yake
umemwezesha kuwa tajiri mkubwa anayemiliki miradi mbalimbali mikubwa ikiwa ni
pamoja na majumba, mahoteli, na miradi mbalimbali iliyotapakaa Marekani,
Mumbai, Istanbul na Ufilipino.
Utajiri huohuo umemfanya tangu mwaka 1996 hadi
2015 kuyamiliki mashindano ya urembo ya Miss Universe, Miss USA, na Miss
Teen USA.
Pia amewahi kuandika vitabu kadhaa na ana
biashara ya kuuza tai na maji ya kwenye chupa kwa kiwango cha kimataifa na
gazeti la Forbes limeuweka utajiri wake katika kiwango cha Dola za Marekani
bilioni 3.7 japokuwa yeye kila mara amesema utajiri wake ni Dola za Marekani
bilioni 10.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv