Karibu katika makala
za kila siku kutoka hapa edonetz na leo tuangazie hili ..Inashauriwa
kwa mwanawake kusitisha kwa muda purukushani za huba pindi atakapobaini
kuwa mwenza wake anavuta kasi ya kuongeza gia. Isitoshe dondoo za
mazungumzo zinashauriwa sana kuchukua nafasi, isiwe ni kasi kwa kwenda
mbele kana kwamba mapenzi ni mchezo wa kukomoana au ni pambano la kumpata
mshindi. Mapenzi hayako hivyo na sio lazima yafanyike kwa mhemko mkali
kwa kipindi chote kana kwamba ni mbio za mita mia.
Pamoja na hayo
wanawake wanashauriwa kutoa angalizo la umbali wao katika kufikia kilele
ili kumpa fursa mwanaume naye kupata kipimo cha wakati wa kumaliza.
Angalizo hilo litamsaidia kumfanya apoteze mawazo kwa hofu ya kuonekana
hafai kwa kitendo cha kumwacha mwenzake njia panda. Ukweli kwa hili sio
tatizo kubwa linalohitaji tiba ya matatibu kwa kiasi hiki, isipokuwa ni
kupata elimu ya kutambua uwezo wa miili yetu.
Hebu soma haya maelezo
ya dondoo zifuatazo yanaweza kukusaidia mwenye tatizo hili.
HAMASA
KUSHUKA:
Upofu mwingine wa
kimawazo ni kwa wanaume na wanawake kutotambua kuwa hamasa ya kimapenzi
hushuka kulingana na muda wa
wapendanao kuwa pamoja. Kuna wengine wanadhani kuwa watadumu kwenda mara sita au saba kama walivyokuwa wakati wa uchanga wa penzi lao.
wapendanao kuwa pamoja. Kuna wengine wanadhani kuwa watadumu kwenda mara sita au saba kama walivyokuwa wakati wa uchanga wa penzi lao.
Katika hili unapaswa
kutambua siku zote mwili wa mwanadamu una desturi ya kuzoea kile
ambacho kinafanyika kila siku. Hivyo basi kabla ya kwenda hospitali
au kubwia madawa ya kuongeza nguvu jiulize maswali juu ya mazoea yako. Na
kama ukitaka kubadilisha mazoea hayo kumbuka kuwa haitakuwa jambo la leo
bali litachukua muda kuliwekea kumbukumbu katika mwili wako.
MAZOEA
YA MWILI:
Watu wengi wenye
majukumu hujikuta wakiizoeza miili yao kwa kufanya mapenzi kwa tendo moja
kutokana na kukosa nafasi, kwao kukutana na mwanamke kwa maana hiyo miili
yao hukosa hamasa ya kurudia kutokana na mazoea. Hivyo muhusika anapotaka
kwenda raundi nne lazima aanze kuuzoeza mwili kidogo kidogo asifikiri
atakurupuka mara moja na kwenda mara tano.
UMRI
WA MTU:
Kuna baadhi ya wanaume
wengine wa ajabu sana; wanajikuta wakihangaika kutafuta dawa za nguvu za
kiume eti kwa sababu hawaendi kama zamani ilhali wanajua fika nguvu za
mwili hupungua kutokana na umri unavyokwenda.
Mwisho..
Ushauri wangu kwako
kama una tatizo hilo basi jitaidi kwanza ujue tatizo liko wapi kasha chukua
hatua anza kulifanyia kazi itakusaidia sana Lakini pia usikubali kukata tamaa
na kujiona huwezi eti kwa sababu umekutana na mwanamke fulani na umeshindwa
kufanya hivyo.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv