Karibu sana msomaji wa edonetz katika mada ya leo ili tujuzane juu ya
hili la leo ikiwa ni kuzungumzia mahusiano tuanzie hapa.
Upo uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa. Kuna
wengine hawana sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na
kile kilichomo ndani ya nafsi zao.
Unaweza kujiuliza; Kwa nini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na
mwenzako? Iwe wa kirafiki au
kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu mbalimbali zinazoweza
kuwafanya wahusika kuamua.
Yawezekana uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako wa jinsia tofautiikiwa
unaona anakutia hasara, au anakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii, au pengine uaminifu wako kazini.
Mathalan, mpenzi wako anafahamika kuwa ni kahaba. Inawezekana uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano,
mwenzio ana nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote analokwambia. Pengine kutokana na hali
hiyo umekuwa ukilazimika kufanya mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na
maadili.
Lakini pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako. Mazingira
yamebadilika, kwa hiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua
kwamba ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!
Uhusiano wowote unapoyumba, uwe wa kirafiki au kimapenzi, huwaweka wahusika
katika wakati mgumu kiasi kwamba ni lazima mmoja achukue hatua ili aweze kuishi
kwa amani na furaha ya kweli.
Hata hivyo, ikae akilini kwamba inauma mno kuachana na mtu unayempenda!
Kumaliza uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni
kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa namna
yoyote.
Kwa leo naishia hapo lakini ukigundua baadhi ya
vitu kama hivyo chukua hatua ndugu..
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv