Mara nyingi tunaona nyoka anatumika katika nembo mbalimbali
dunia ni sasa iko hivi Nyoka anatumika
kwa sababu ya maisha halisi ya mnyama huyu ambaye baada ya muda katika maisha
yake huwa anavua gamba na kuota tena kuwa kitu kipya; maana yake ni maisha
mazuri, maumivu wakati wa kuvua gamba na uponyaji wakati anapoendelea na maisha
ya baadaye.
Kwenye huduma za matibabu na baadhi ya majeshi utaona fimbo
iliyozungukwa na nyoka, utaweza kuikuta kwenye hospitali karibu zote, huduma
zote za afya na sehemu nyingine nyingi fimbo hii ni alama ya Kigiriki
iliyotumika kwa maelfu ya miaka inaitwa Rod of Asclepius au Staff of Asclepius. Ni fimbo ya Mungu
wa Kigiriki anayeitwa Asclepius anayehusishwa na
mambo ya uponyaji na matibabu.
Aesculapia ni nyoka waliokuwa wanatumika katika mahekalu ya
kutolea matibabu, nyoka hawa walikuwa huru katika vyumba vya wagonjwa waliokuwa
wamelazwa ndani toka mwaka 300.
Lakini kwa tamaduni za Wahindu suala hili limeenda mbali zaidi
katika kueleza mfumo wa vyakula, maisha, matibabu ya asili na mengine mengi.
Sehemu kama Thailand nyoka wa aina hii hutumika sana kwenye
matibabu ya misuli, mishipa, msongo wa mawazo na aina nyingine ya maliwazo.
Kwa Afrika ni ngumu kidogo maana elimu nyingi za kale zilifutwa
baada ya ujio wa utumwa na ukoloni na hata sasa hakuna wenye hamu ya kufahamu
mambo mbalimbali kuhusu nyoka na jinsi wanavyoweza kutumika kwenye shughuli zao
za kila siku hasa matibabu na uponyaji.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv