edonetz itazidi kukuletea kila siku makala zinazohusu afya, malezi, mausiano, siasa, burudani.. nk na siku ya leo nimekuandalia lishe bora kwa mtoto umri kuanzia miezi sita kushuka chini..
UMRI KUANZIA MIEZI SITA KUSHUKA CHINI
Kwa watoto walio chini ya umri wa miezi sita, wanatakiwa wapewe maziwa ya mama pekee, mtoto asipewe kitu kingine chochote kile katika umri huo (hata yawe maji).
Hii ni muhimu sana, kwani maziwa ya mama yana kila aina ya kirutubisho ambacho mtoto huyu anahitaji katika umri huu na hakuna mbadala wake, hata kama mama anakwenda kazini, basi anaweza kumkamulia mtoto maziwa na yakahifadhiwa vizuri, kwenye chombo kisafi, maziwa ya mama yakikamuliwa, yana uwezo wa kukaa hadi masaa 6 bila kuharibika (hata yasipo hifadhiwa kwenye friji) na yakihifadhiwa kwenye friji, basi yanaweza kukaa hata kwa masaa 24.
Kuna tabia pia ya wazazi kuwapa watoto chini ya miezi 6 maji, hii pia si sahihi hata kidogo, kwani maziwa ya mama yana kiasi cha maji cha kutosha sana, mtoto anapoonekana kuwa ana kiu, basi anyonyeshwe na sio kupewa maji, kuanza kumpa mtoto chakula cha aina nyingine ambacho si maziwa ya mama, ni hatari kwa afya ya mtoto kwa sababu tumbo lake bado halijakomaa vya kutosha, na inaweza kusababisha maambukizi kwenye tumbo, tumbo kujaa gesi na hata kuharisha.
Kama mama hatoi maziwa ya kutosha, ajitahidi kuendelea kumpa ziwa mtoto, kwani kadri mtoto anavyovuta ndivyo ambavyo maziwa yanazidi kutengenezwa kwa wingi zaidi, na mama akipunguza/akiacha kumpa mtoto ziwa basi maziwa yanakuwa yanatengenezwa kwa kiasi kidogo sana.
Pia mama ajitahidi kunywa maji sana (angalau lita tatu au zaidi kwa siku), na vyakula vya majimaji vya kutosha ili maziwa yatengenezwe kwa wingi, madaktari hawashauri sana maziwa ya formula, kwani hayafikii ubora wa maziwa ya mama, lakini, pale inapobidi, kutokana na maisha tunayoishi sasa mama anaweza asipate maziwa ya kutosha, na kama ana uwezo basi anaweza akamnunulia mtoto wake maziwa ya formula, ili kuongezea.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv


 
Top