Malezi ya
mtoto yatakuwa mazuri katika maisha yake yote endapo atapata malezi mazuri kutoka
kwa wazazi wote wawili yaan baba na mama na endapo mtoto atakosa malezi kutoka
upande mmoja basi kisaikolojia basi kalibu leo tuongelee hili kwa kina siku ya
leo
Kwanza tuangalie Mzazi
mmoja ni nani? ni mtu ambaye ametengana na mume au mke na kuachiwa
malezi ya watoto peke yake. Pia mzazi mmoja anaweza kuwa mwanamke au msichana
aliyepata ujauzito bila kufunga ndoa, hapa anaweza kuwa mwanafunzi wa
sekondari, shule ya msingi au wa Chuo Kikuu. Pia kwa maisha ya siku hizi
wanawake wenye uwezo kimaisha hupendelea kulea watoto wao bila msaada wa
mwanaume aliyezaa naye kwani wengi wao hukwepa kuingia kwenye maisha ya ndoa
kwa sababu mbalimbali.
ATHARI ZA KISAIKOLOJIA
Uchunguzi uliofanywa na wanasaikolojia umebaini kuwa mtoto
mwenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano hasa wa kiume huwa karibu sana na
mama na watoto wa kike wenye umri huo pia huwa karibu zaidi na baba, kutokana
na ukaribu huo watoto hao watakuwa na mapenzi hata wakija kuingia kwenye
mahusiano pale wanapokuwa wamevunja ungo au kubalehe hukosa uelekezi mzuri
kwenye tabia chanya.
Kukosa ukaribu;
watoto hasa kwenye kipindi cha kubalehe au kuvunja ungo ndio athari
zinaanza kujionesha kwani kuna vitu ambavyo anatamani kumueleza na mzazi husika
kama ni baba au mama ili kuweza kupata taarifa husika, lakini pale anapokosa
maelekezo ya mzazi ananza kutafuta taaarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii
ambayo itamsababisha kutopata uhalali wa jambo analotarajia kulifahamu.
Athari ya kiuchumi;
hapa anazungumziwa mzazi asiye na uwezo wa kutimiza mahitaji ya
mwanae kutokana na kudorora kwa uchumi ambapo hupelekea mtoto kuathirika
kisaikolojia kwa kukosa mahitaji muhimu shuleni kama viatu, sare za shule na
ada. Hali hii inayompelekea unyonge mtoto huyu kitaalamu huitwa (Inferiorty
Conflict) ambayo huathiri namna ya kujifunza.
Kupata kasoro za kisaikolojia kwenye jamii;
hapa mtoto ambaye anapata malezi ya mzazi mmoja anakosa kujiamini
hata mbele za watu kwani hakupata malezi ya pande zote mbili hali
inayochangia kufifisha uwezo wake wa kujiamini.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv