Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana .unaweza kujiuliza Nini nifanye ili nipate mtoto wa kike au kiume? Je kuna dawa au vyakula vya kusaidia kupata mtoto ninayemtaka?Siku gani nikikutana na mwenzangu naweza pata mtoto wa kiume au kike?
Na maswali
mengine mengi huonesha shauku kubwa ya kupata mtoto wa jinsia uipendayo. Tuanzie
hapa.
Tuanze na Jinsia ya Mtoto
Mtoto
hutengenezwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la kike. Mbegu za kiume
hubeba vinasaba vya X na Y, wakati
yai la mwanamke likiwa na vinasaba vya X peke. Ikikutana mbegu ya kiume yenye
kinasaba cha X na yai la kike (yenyewe yana vinasaba vya X peke
yake) mtoto wa kike hutungwa. Mbegu ya kiume yenye kinasaba cha Y
Ikikutana na yai la kike, mtoto wa kiume hutungwa.
(Mbegu ya kiume
Y + Yai la kike X = Mtoto wa Kiume)
(Mbegu ya kiume
X + Yai la kike X = Mtoto wa Kike)
Na hizi ni Njia za Kupata Mtoto Wa
Jinsia Uipendayo
Mbegu za kiume
zenye vinasaba vya Y huwa ni nyepesi, husafiri kwa haraka katika via vya uzazi
vya mwanamke na huishi kwa muda mfupi ukilinganisha na mbegu zenye vinasaba X.
Zenye vinasaba X huwa nzito zaidi, huenda polepole na huishi kwa muda mrefu
zaidi.
Hivyo,
kinadharia ili kupata mtoto wa kiume unaweza ukakutana na mwenza wako siku
ambayo yai la uzazi linatoka (ovulation), kwani mbegu Y
zitasafiri haraka na kukutana na yai ili kulirutubisha kuwa mtoto wa kiume.
Mtoto wa kike,
kutana na mwenzi wako siku 2 au 3 kabla ya yai kutoka. Kwa sababu mbegu Y
huishi kwa muda mfupi, nyingi zitakufa wakati zinasubiri yai huku mbegu X
zikiwa kwa wingi mpaka siku yai linatoka. Yai likitoka mbegu X zitakuwa kwa
wingi kuungana na yai kutunga mtoto wa kike.
Kiuhalisia, sio
rahisi kufanikisha hilo.
Na kwa wakati mwingine waweza kufanya
hivi
Kuna njia
mbalimbali zinazosemekana zinaongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume au kike.
Njia hizi inajumuisha kula vyakula vya aina fulani, mikao maalumu ya kimapenzi,
kuweka vitu sehemu za siri na nyingine nyingi bado haziwezi kutatua tatizo
hili.
Mpaka sasa na
maendeleo yote ya kiteknolojia hatujaweza kupata njia ya kuwezesha kupata jinsia
ya mtoto unayoitaka. Ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu!
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv