Imekuwa ni kawaida kuona wale wasichana au akina mama ambao wana akili nyingi hawaolewi tunaona wanaishi pekee yaan cingel uenda unajiuliza kwa nini inakuwa hivyo kwa kawaida Akili nyingi ni zawadi kutoka kwa Mungu lakini wataalamu wanasema zikizidi huwa ni tatizo katika mahusiano kwani wanapojiangalia kwenye kioo, wanawake wenye akili nyingi huona picha ya mtu mwenye nguvu mwenye malengo, anayejua anachotaka. Kuwa na akili nyingi ni kitu muhimu kuwa nacho, lakini wakati mwingine kinaweza kuwatisha wengine. ndio maana watu wenye akili nyingi hupata shida ya kupata pendo, kama unajiuliza kwanini bado upo single, hizi ni sababu tano kwanini unaweza ukawa unapata shida kupendwa.
Hizi ni miongoni mwa sababu hapa…
Unakuwa mchambuzi mno
Wasichana wenye akili mara nyingi huchambua sana vitu. Huwa na shaka na kesho yao, njia nzuri ya kuimarisha mahaba, na wanataka sana kumpata mtu sahihi, hata hivyo hiki sio kitu kibaya.
Unajua ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mwenza asiye sahihi
Hakuna tatizo katika hili pia, watu wenye akili wako makini katika kumpata mwenza sahihi ambapo wanaweza kuamua kubaki wenyewe kama asipopatikana.
Unajua kuwa mahusiano mara nyingi hufa
Hawa hujua ukweli unaouma kuwa mahusiano mengi hayafiki popote, matokeo yake wakati mwingine hufanya mambo pole pole na kuwa na shida katika kuingia miguu miwili, lakini mwenza sahihi ataelewa hilo.
Unaweza kuwa unaogopesha
Sio kwamba watu wenye akili huwatisha mambumbumbu lakini hata wenye akili pia. Wanaweza wasiwe na ukweli kuwa unafanya vizuri katika eneo la maisha ambayo hawapo.
Unajua kujilinda mwenyewe
Watu wenye akili katika dunia hii wanaelewa hatari katika hali yoyote na hiyo inahusisha pia mahusiano, huwa makini, waangalifu na huweka vikwazo kujilinda wenyewe.


JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top