NA christian ignas -EDONETZ


Ligi ya TFF U20 kituo cha Dar es Salaam, itafanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, badala ya Uwanja wa Uhuru. Sababu ni kuwa Uwanja wa Uhuru utakuwa ukitumika kwa   mazoezi ya gwaride la kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru. Kiingilio kwenye mechi hizo ni Sh. 2,000 ambako kesho kutakuwa na mchezo kati ya Simba na Ndanda saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni JKT Ruvu na Ruvu Shooting. IMETOLEWA NA TFF.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Samir Nasri: Guardiola huwataka wachezaji kutofanya mapenzi baada ya saa 6 usiku.

Mchezaji wa Ufaransa katika safu ya kati Samir Nasri amefichua kwamba mojawapo ya ufanisi mkubwa wa mkufunzi Pep Guradiola ni kuwaagiza wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya saa sita usiku.
Katika mahojiano na runinga ya Ufaransa,Nasri amesema kuwa Guardiola aliweka sheria hiyo hata iwapo kungekuwa hakuna mechi siku iliofuatia ili wachezaji wapate usingizi mwanana.
Hata Lionel Messi anayetambulika kuwa mchezaji bora duniani hakuwachwa nje wakati wa uongozi wa Guradiola katika timu ya Barcelona.
Nasri amesema kuwa hatua hiyo ilimwezesha Messi kutopata majeraha ya misuli
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kiungo wa kati wa zamani wa England na Chelsea, Frank Lampard amesema ataiaga ligi ya MLS ya New York City.

Lampard mwenye umri wa miaka ,38, ambaye mkataba wake utakamilika mwishoni mwa mwaka huu , amechapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba wakati wake katika klabu hiyo ''umefika kikomo.''
Amesema atatangaza hadharani ' hatma yake ya siku zijazo' hivi karibuni.''

Lampard amefunga mabao 15 katika mechi 31 alizoshiriki katika klabu ya New York ,kwa miaka miwili iliyokatizwa na mkopo kutoka Manchester City.
New York City walifungwa mabao 7 kwa nunge na klabu ya Toronto FC katika hatua za kwanza za mwezi.
Lampard alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2014, na kuvunja rekodi ya mabao 211.
Mwenzake wa timu ya timu ya Uingereza na Liverpool Steven Gerrard pia anaweza kumaliza muda wake nchini Marekani

Gerrard, 36, amesema amekamilisha mkataba wake kwa akiichezea klabu ya LA Galaxy na amesema anaweza kuhudumu kama mkufunzi kwa klabu yake ya Liverpool.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top