Katika mfurulizo wa makala zetu acha
leo tuongelee mausiano kwa mala nyingine tena…. Mapenzi ni kitu Fulani tofauti
sana kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana
yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti
hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi,
kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida
kisa mapenzi.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza
kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata
kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi
zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye
mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa
sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa
wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana
haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote
lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua
unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye
mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo
kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile
vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi
kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila
kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye mapenzi kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa
dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya
wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa
inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa
bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye
mapenzi.
4. DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa
kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano
jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata
kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu
mwenye dharau hata awe nani. Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana
akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara
nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao
kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La Ndoa/Kuishi
Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke Kama Ndio
Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi
Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha
Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea
ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.
5. MROPOKAJI/ASIYE MSIRI.
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya
mwenza wako kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua kama
wewe ni mropokaji na huna ‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani
na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na
huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda
kusimulia. Mambo mnayafanya mkiwa
wawili tena ndani lakini kesho unaenda mtaani unakuta kila mtu anajua
mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo vile, hiyo si kitu nzuri na
itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.
6. TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya
mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye
mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa
na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika. Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua
kuwa naye basi usiwe na tamaa kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia
mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu
kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya
lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi
nyepesi zinazoweza kuku-cost hapo baadae.
7. KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye
mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia
pamoja na teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye
mitandao na vyombo mbali mbali vya habari. Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na
unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa hawafahamiani
huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza
sana na kupelekea kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi
haa duniani. Kama kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo
na umjali na kumchukulia kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia
majukumu bila sababu zote za msingi. Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye mahusiano ni bora
ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.
9. UBAHILI.
Huna sababu yoyote ya kuwa na pesa na
mpenzi wako akawa anapata tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa
mambo yasiyo na msingi lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako
kila unapohitajika. Kuna vitu vingine hata
huhitaji kuambiwa kama unatakiwa kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa
responsible kumhudumia mpenzi wako. Na hii huwa ina-apply sana kwa wavulana
kutokana na kasumba iliyojengeka na mila tulizozikuta.
10. USHOGA/USAGAJI
Hii ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu
anayependa mtu wake awe Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana.
Ni aibu kubwa sana kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani
kwa akili ya kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama
utakishuhudia kwa macho yako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv