Na christian ignas - edonetz



Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na viwango vya baadhi ya nyota waliokuja kufanya majaribio ya kujiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo uliofunguliwa leo.

Azam FC jana usiku ilimaliza programu ya kukifanyia tathimini kikosi chake kwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-1 kwenye mchezo wa kujipima ubavu, ambao pia iliutumia kuwapima wachezaji tisa waliokuja kwa majaribio, mabeki wa kati Nkot Mandeng Eric (Coton Sport De Garoua, Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Asec Mimosa, Ivory Coast).

Kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Coton Sport Garoua, Cameroon), Abdallah Khamis pamoja na washambuliaji Yaya Anaba Joel (Coton Sport Garoua, Cameroon), Samuel Afful (Sekondi Hasaacas, Ghana), Bernard Ofori (Medeama, Ghana), Konan Oussou (Tala’ea El-Gaish SC, Misri) na Jean Karekezi.

Mabao mawili kati ya matatu ya Azam FC usiku wa jana yalifungwa na nyota waliokuwa majaribio, ambao ni Ofori aliyefunga la kwanza kwa kichwa akimalizia krosi safi ya Gadiel Michael na Afful akitumia juhudi binafsi kwa kumzidi maarifa beki pemmbeni ya uwanja na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Beki wa kagera asubiri hukumu ya kusimamishwa
Beki wa Kagera Sugar Erick Kyaruzi 'Mopa' amesema anaumizwa na tuhuma za kusimamishwa kuichezea timu hiyo na kuuomba uongozi kulimaliza suala hilo.
Mchezaji huyo sanjali na kipa Hussein Sharrif walisimamishwa kuichezea timu hiyo mwezi uliopita kwa madai ya kuihujumu klabu hiyo hadi ikaambulia kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa Yanga.

Akizungumza na mwandishi wetu Kyaruzi alisema anaamini hana hatia kwa kuwa hajawahi kufikiria kuihujumu timu hiyo tangu aanze kuitumikia miaka minne iliyopita.
"Nimesimamishwa lakini ninaumia kwa sababu soka ndio ajira yangu,sijawahi kufikiria kuihujumu Kagera katika maisha yangu,"alisema 
Kocha mkuu wa Kagera Maecky Maxime alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa lipo katika uongozi.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top