Walio wengi wanachukulia kawaida lakini Kumtongoza mwanamke sio jambo la mchezo kunahitaji ufundi wa aina yake ambao usipozingatia utakosa fursa ya kumpata umpendaye hivyo Mtembezi Mahaba inakuletea baadhi ya mambo ambayo hufai kuonesha wakati wa kumtongoza mwanamke.
1.PAPARA.
Wanaume wengi wamekuwa na haraka wanapokuwa wakitongoza hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu, mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake, mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata kwa kuwa  atakufikiria sana juu ya uharaka wako.
2.KUJIKATAA
Wanaume wengi wamekuwa wakijipandisha au kujionyesha tofauti na hali walizonazo, ukiwa unatongoza jifunze kuwa mkweli kwani ukweli ni moja ya vigezo ambavyo wanawake huvipenda kwa mwanaume.
3.KUTOSOMA ‘MOOD’ YA MWANAMKE
Unapomtongoza  mwanamke lazima usome yuko katika hali gani kwa kuwa unaweza kutoswa kwa sababu tu hujamsoma mwanamke, huenda akawa na hasira akakujibu vibaya hivyo ni vyema kumsoma kwanza.
4.KUMPONDA MPENZI WAKO WA AWALI
Mwanamke anakuuliza kwanini uko ‘single’, unaanza kumponda ‘ex’ wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae kwani anaweza fikiria kuwa akikukubalia mkaachana unaweza ukamfanyia kama ulivyomfanyia mpenzi wako wa awali.
5.KULALAMIKA
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako, jikubali utafanikiwa kupata mwenza wa maisha yako
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top