SIO kitu kigeni katika maisha ya
kila siku kukumbana au kukutana na watu wenye matatizo haya ya kukoroma
haijarishi ni mwanaume au mwanamke na hili ni miongoni mwa vitu vinavyochokera
kupita maelezo ni pale inapotikea unalala na mtu anayekoroma. ASEE Inakera
kweli kweli kwani kelele za mtu anayekoroma hukosesha wengine kufaidi raha ya
usingizi kwa sababu ukweli ni kwamba ukiachilia mbali raha ya kujinyoosha
pia usingizi una raha yake asikwambie mtu;
Basi inapotokea mtu akakukatisha
raha hiyo huwa tafrani tupu. Watu wengi wana tabia ya kukoroma wanapolala,
lakini kukoroma siyo kuzuri sana kwani familia yako pengine hushindwa kupata
usingizi vizuri kutokana na makelele yanayotokana na kukoroma kwani maana
halisi ya kukoroma kunamaanisha kuwa pumzi zako haziko sawa, wataalamu wa
masuala ya afya wanasema wakati mtu anapokoroma kunaweza kusababisha kukosa
pumzi na kupelekea kifo.
kumbuka mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya
kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu
wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni
zake.
Tatizo hili linaweza
kuisha kabisa baada ya wiki 2 unatakiwa
kuendelea na mazoezi hata mara mbili kwa
wiki ili misuli isilegee tena.
ZINGATIA YAFUATAYO…
Kwa hivyo, zifuatazo ni ‘tips’
kadhaa zitakazokusaidia kubadilisha hali hii.
· Kwanza kuchagua
mito laini inayoweza kufanya shingo yako iwe vizuri, ambayo itakusaidia kupumua
vizuri.
·
Pili tumia mashine ya (humidifier) ili
hewa ndani ya chumba iwe ya unyevu na kukusaidia koo lako kutokuwa kavu.
· Tatu,
kunywa asali kidogo kulainisha koo lako na usinywe pombe kwani inapandisha
shinikizo la damu na kuwa juu hivyo kusababisha koo lako kubana na kuzuia
kupata pumziNne, ambalo ndilo jambo la msingi kabisa linalosisitizwa na
wataalamu wa afya ni kufanya mazoezi mara kwa mara ! Mazoezi ni dawa
iliyothibitika kutibu magonjwa mengi.
FANYA
ZOEZI HILI ITAKUSAIDIA SANA..
Fungua mdomo wako mpaka
mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka
mwisho-rudia mara 20.
Ukimaliza utahisi kuna
misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio
inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili
litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv