Ukiongelea vitu vitamu zaidi duniani lazima utaje na asali
ambayo inatengenezwa na wadudu aina ya nyuki ambao wanachanganya vitu mbali
mbali kama ifuatavyo…
Asali hutengenezwa na nyuki wanaotumia ‘vumbi’ maalum la
maua liitwalo nectar. Kiwango cha
sukari katika asali ni asilimia 70 hadi 80 na kiasi kinachobaki ni maji,
madini na huwa na kiwango cha protini, asidi na vitu vingine.
Asali imekuwa ikitumika kwenye matibabu ya vidonda, matatizo ya
ngozi na magonjwa tofauti ya tumbo na ina uwezo wa kuua bakteria mwilini.
Pamoja na uzuri na utamu wa asali lakini pia ina madhara yake
kwani inaweza kuongeza uwezekano wa kutokwa damu, ikiliwa pamoja na
dawa zinazoyeyusha damu kama vile Asprini, dawa za kuzuia damu kuganda
kama Warfarin (Coumadin), Heparin na
kadhalika.
Asali pia inaweza kushusha kiwango cha sukari mwilini, hivyo
lazima kuwe na tahadhari ya matumizi yake kwa mtu mwenye ugonjwa wa
kisukari anayetumia dawa zinazoshusha sukari mwilini kwa sababu zikitumika
kwa pamoja huweza kusababisha kushuka sana kwa kiwango cha sukari na
kuleta hatari ya kifo au kifafa kwa mtumiaji.
Asali pia inaweza kuingiliana na dawa zinazofanya kazi kwa
kutumia kimeng’enya mwili cha Cytochrome p450 kinachofanya
kazi ya kuvunja dawa na hivyo huweza kufanya dawa ifanye kazi kwa
kiwango kidogo ama kufanya kazi kwa kiwango zaidi ya kile kilichokusudiwa
hivyo kuwa sumu ama kutomsaidia mtu.
Inashauriwa mtumiaji wa dawa hizo aonane na mtaalam wa afya
ili amueleze kama ni salama kunywa dawa zinazohitaji kimeng’enya hiki
katika utendaji kazi mwilini pamoja na asali kwa usalama wao.
Asali pia inaweza kuingiliana na dawa za damu, moyo, mfumo wa ufahamu, ngozi,
tumbo au matumbo, fangasi, mfumo wa mkojo, saratani, kifafa, kupunguza
lehemu, meno, pombe, kupunguza uzito na dawa za kutibu vidonda. Asali pia inaweza
kushusha shinikizo la damu mwilini, hivyo wagonjwa wanaotumia dawa za
kushusha shinikizo la damu la juu (High Blood
Pressure), wanapaswa kushauriana na madaktari wao kabla ya kutumia.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv