hapa duniani kila mtu alikuja peke yake na kila mtu anakula kwa jasho lake hivyo hivyo katika kazi na kipato ni tofauti hata maisha ya kawaida yanakuwa tofauti karibu tunaendele na mada zetu na leo tutaangalia makundi manne ya watu katika dunia.
1.WANAMUDA LAKINI PESA HAWANA
Hili ni kundi ambalo watu hawa wanamuda wa kutosha kufanya mambo mengi sana lakini pesa hawana hata kama kuna usemi unasema muda ni mali, hawa utakuta kazi zao ni kuangalia TV muda mwingi, kupiga story, au kutembelea sehem zinazopoteza muda, siumewahi kuwaona wafanyakazi ambao wanamuda wa kutosha wanatoka kazini saa nane, saa kumi au saa saba, wanamuda wa kutosha lakini pesa hawana.ukiwa hapa usipojitambua ukatoka kwa kutumia muda wako wa ziada huo kufanya ya ziada umeumia.
2.WANAPESA LAKINI MUDA HAWANA
Umewahi kumsikia mtu anatoka nyumbani saa kumi na moja kuwahi kazini, anarudi nyumbani saa nne usiku na akifika nyumbani anamalizia kazi za ofisini, yani yuko bize muda wote, hana muda wa kukaa hata na familia yake, hana muda hata wa kufurahia ndoa yake, hana uhuru wa muda, japo analipwa mshahara wa kutosha na anacheo kikubwa.Hawa huwa ni watumwa wa pesa hawako huru.
Mwisho wa siku ni kupata magonjwa
3.WANAMUDA NA PESA WANAZO
Kundi hili ni kundi la neema, ni kundi ambalo watu pesa wanayo na muda wanao, hebu nikutolee mfano mwanamuziki diamond anafanyakazi usiku mmoja anaingiza zaidi ya milioni tano, huyu anauhuru wa pesa na muda, anaweza kesho kusema napumzika naenda swimming, hebu muangalie Mengi, Bakhresa, Erick Shigongo n.k, hawa wanaweza kwenda rikizo saa yoyote kwasababu wanapesa na muda wanao hata familia zao zinawatambua, lakini hebu niangalie na mimi hahahaa naamka saa nne ndo naenda kazini, saa tisa nimemaliza kwasababu Neptunus inanipa uhuru wa muda na fedha ambao kutegemea ajira ingekuwa ndoto.ili uwe kundi hili uwe mfanyabiashara tena wa biashara ya karne ya 21 au uwe na kipaji.Watu hawa wanamuda wa kuhudhuria mafunzo na semina mbalimbali.hawa wanauhuru wa muda na fedha
4.HAWANAMUDA NA PESA HAWANA
Kuna watu maisha yao yoote wako bize na ubize huo hauwafanyi waongeze kipato, mtu anatoka kazini saa kumi anakwambia siwezi kufanyabiashara sina muda, mtu anatoka kazini saa nane anakwambia sina muda, watu hawa banah huwa kama hawajielewi fulani hivi, hana muda lakini muulize anaongeza kipato chake au haongezi, watu hawa hata umwambie kuna semina bure atakwambia sina muda, hata umwambie nakupa kitabu bure usome hana muda, mwisho wake ni kufa masikini.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top