LEO nimeona hata akina dada zangu nisiwasahau saana nigusieb katika urembo kwa kuangalia  njia sahihi ya kukuza nywele na kuzifanya ziwe ngumu, zisikatikekatike pia kuzipa rangi halisi. Kuna wanawake kutokana na kupakapaka madawa nywele zao hupoteza rangi wengine huwa na nywele nyekundu kama zilikuwa nyeusi.
Katika mazingira hayo unaweza kutumia vifuatavyo;
Baking soda
Inatumika baada ya kusafisha nywele zako na kuwa safi. Unachukua vijiko vitatu vya chai vya baking soda, unachanganya na maji kisha unaoshea nywele.Hii inasaidia kuleta rangi halisi ya nywele.
Asali na mafuta ya mzaituni
kama utakuwa na tatizo la muwasho au kupata tatizo lolote kichwani huenda nywele zinakatika bila wewe kujua, tumia vitu hivyo vitakuweka sawa.
Chukua asali changanya na mafuta ya mzaituni. Chukua nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni, changanya na vijiko viwili vya asali vidogo kisha paka eneo lenye tatizo, acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha kwa maji ya baridi.
Nikisema sehemu yenye tatizo namaanisha kama nywele zimepukutika au una mba wanaosababisha unajikuna sana nk.
Papai
linasaidia pia wanawake wengi wakishaweka dawa kichwani huwa wana tabia ya kutaka kuzikata ili wazilinganishe huko saluni, lakini steaming hii ya papai ambayo unaweza kuifanya nyumbani kwako inao uwezo wa kuzifanya nywele zako zilingane.
Jinsi ya kutumia Chukua yogati kipande na papai nusu, vichanganye pamoja kisha baada ya hapo paka mchanganyiko huo kwenye nywele zako, acha kwa muda wa nusu saa na baada ya hapo osha kwa maji ya vuguvugu.
Nywele ndefu kwa ujumla kupata nywele ndefu chukua yai moja, mafuta ya mnyonyo vijiko vitatu na kijiko kimoja cha siki ya tufaha, changanya kwa pamoja kisha paka nywele zako acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha.”


JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top