miongoni mwa matatizo yanayowakumba akina mama hasa wakati wa uzazi hili nalo ni kubwa ingawa kuna matatizo mengi ambayo unatakiwa kuyajua lakini kwa kwa leo acha tuanze na hili, Kuna
tatizo la upevushaji mayai. Tatizo hili kitaalamu linaitwa ‘Ovulatory Factor’,
husababishwa na kasoro mbalimbali kwenye mfumo wa homoni ambao hutokana na
uwepo wa uvimbe katika ubongo, kuwa na upungufu katika mfumo wa homoni, uvimbe
wa vifuko vya mayai, vifuko vya mayai kushindwa kuzalisha vichocheo au mayai
yenyewe, kuchelewa kwa mwili wa mwanamke kupevuka na magonjwa mbalimbali pamoja
na unene kupita kiasi.
Matatizo
haya huambatana na dalili mbalimbali, kutegemea na jinsi tatizo linavyotokea,
mfano kutokuota vinyweleo sehemu za siri na kwapani, kutokuota matiti au
kuchelewa kupata mabadiliko hayo. Kuota ndevu na vinyweleo mikononi na miguuni,
hata tumboni na kifuani kwa wanawake. Kutokupata damu ya hedhi kabisa au kufunga
kupata kwa muda mrefu.
Matiti
kutoa majimaji au maziwa, kupoteza hisia na raha ya tendo la kujamiiana. Kwa
hiyo mwanamke anaweza kuwa na zote au mojawapo ya dalili hizo kutegemea na
athari zilizojitokeza kwake.
Kuna
matatizo ya nyonga ambayo yapo chini ya tumbo usawa wa kitovu ni mojawapo ya
matatizo makubwa yanayoathiri uzazi kwa mwanamke.
Lakini
maambukizi mbalimbali, mfano ugonjwa wa kidole tumbo ambao wengi wamezoea kuita
“Apendix’ lakini kitaalamu unaitwa ‘Appendicitis’ huweza kusababisha mwanamke kuwa
na maumivu makali tumboni.
Maambukizi
sugu katika viungo vya uzazi au ‘PID’, kushikamana kwa kizazi kutokana na
makovu yanayosa-babishwa na kusafisha kizazi mara kwa mara na baada ya mimba
kuharibika au kudhani kwamba ni msaada wa kuharakisha kupata mimba, kasoro
katika tabaka la ndani la kizazi kuwa nje ya kizazi, uvimbe wa fibroid pia
huchangia kwa kiasi kikubwa ugumba.
NA sasa hebu tuangazie Dalili za tatizo .
Dalili
kuu za matatizo haya ni maumivu sugu chini ya tumbo, kuvuruga mzunguko wa hedhi
au kutokupata hedhi, maumivu wakati wa tendo la kujamiiana, kutokwa na uchafu
ukeni kwa muda mrefu wenye muwasho na harufu.
Mwanamke
anaweza kuwa na tatizo katika shingo ya kizazi na tatizo hili linaweza kuwa la
kuzaliwa nalo, likasababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa kwa mjamzito, hivyo
kumfanya kuzaa mtoto mwenye kasoro katika viungo vyake mojawapo ni viungo vya
uzazi.
Mwanamke
anaweza kupata tatizo la uzazi kutokana na kufanyiwa upasuaji au magonjwa sugu
katika uke au shingo ya uzazi.
Ukizungumzia
tatizo la ugumba kwa mwanaume na mwanamke lazima kuwepo na uchunguzi wa
kidaktari ili kugundua. Kwa mwanamke mambo ya kuangalia ni historia yake katika
matumizi ya madawa ya tiba, alipokuwa mdogo au hata kama mama yake aliwahi
kutumia aina fulani za madawa wakati wa ujauzito.
Daktari
ataangalia alivunja ungo kwa wakati muafaka, mfano aliwahi sana au alichelewa
sana. Muda muafaka ni kati ya miaka 11, 12 hadi 16. Kufahamu mzunguko wake wa
hedhi unavyoenda na kiwango cha damu unachopata, kama alishawahi kutumia njia
za kisasa za uzazi wa mpango au alishawahi kuzaa au kuharibu mimba.
Vilevile
inahitajika kujua kama ulishawahi kufanyiwa upasuaji wowote chini ya tumbo
mfano kutoa uvimbe, mimba nje ya kizazi, kuzaa mtoto kwa upasuaji. Ni muhimu
pia daktari akafahamu endapo ulishawahi kupata maambukizi yoyote katika viungo
vya uzazi.
Tatizo
hili la kutokupata mtoto au ugumba kama tulivyokwishaona hapo awali, linawahusu
mke na mume, yaani watu wawili wanaotafuta mtoto lakini mimba ama zinatoka au
hafanikiwi kabisa.
Kwa hiyo,
mwanamke mwenye tatizo hili la kutopata ujauzito anatakiwa kwenda kuonana
na madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi na atafanyiwa vipimo vya kisayansi. Ni
vema kwenda wote wawili kufanyiwa vipimo.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv