Watafiti wa masuala ya mahusiano na ndoa wana kalenda za miaka
ya hatari iliyotafsiriwa sambamba na sababu zinazoweza kuvuruga
uhusiano na kuwafanya watu waliokuwa wakipendana kuachana.
Hivyo kwa dondoo tu nimeona ni vyema nikudadavulie watu
wanaoishi kwenye ndoa sababu zinazotafsiri ukomo wa mapenzi yao kulingana
na miaka husika iliyotafsiriwa na watalaamu wa masuala ya ndoa na
mahusiano.
Wanasaikolojia mbalimbali ulimwenguni kupitia tafiti zao
walikubali kuuweka UGOMVI kuwa katika
sababu zinazoweza kusababisha ndoa kuvunjika ndani ya mwaka 1-2. Wanasema endapo watu waliooana
wakianza kugombana kati ya mwezi wa kwanza na kuendelea, basi ujue
kuwa wanandoa hao hawawezi kuvuka miaka miwili kabla ya ndoa yao
kuvunjika.
Jambo la kuzingatia katika sababu hiyo ya ugomvi iliyotajwa ni
kwamba watafiti hao hawachukulii hitilafu na migongano ya kawaida
kama sababu, bali mikwaruzano mikubwa yenye kuumiza mwili au roho kwa
kiasi kikubwa.
Watafiti hao wanasema wanandoa na wapenzi hugombana kwa kipindi
hicho huwa na kasoro ya ulinganifu wa tabia, mawazo na mwelekeo
hivyo kuwafanya wasiweze kuishi pamoja kwa muda mrefu.
Hivyo ili wanandoa wasiweze kuachana katika miaka miwili ya
mwanzo wanashauriwa kuoana baada ya kuchunguzana vema tabia na
kulingana katika hali.
Mwaka mwingine wa hatari ni wa NNE. Baada ya kuoana
mwaka wa nne unatajwa na watafiti kuwa ni wa hatari katika kuwafikisha
wapendanao ukingoni mwa mapenzi yao.
Sababu ambayo inapewa uzito katika kizuizi hiki cha ndoa
ni kufanikiwa kupata MTOTO. Kuwekwa kwa mtoto
katika kizingiti hiki kunaonekana na tafiti nyingi kuonesha kuwa wanandoa
wanapofanikiwa kupata mtoto hujisahau na kuhamisha mapenzi yao kwa mtoto,
huku wakijisahau kuwa wao pia wanajukumu la kupendana.
Watafiti hao wanasema wapendanao wanapokuwa na mtoto, muda
mwingi humfikiria zaidi yeye. Kama ni suala la kuchukua zawadi za kurudi
nazo nyumabani hazitakuwa kwa ajili ya mume/mke bali itakuwa ni kwa mtoto.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv