Karibu msomaji wa edonetz tujadili kwa pamoja leo tuzungumzie umuhimu wa zawadi
katika mahusiano kama utakuwa na lolote tuandikie hapo chini au kama kuna
lolote la kutujuza tujuze tu tutalifanyia kazi.
Tuendelee na mada yetu ya umuhimu wa zawadi katika
mahusiano ya mapenzi kumbuka haijarishi ni zawadi gani...
1. ZAWADI
ZINABORESHA MAPENZI:
Umuhimu wakwanza
wa Zawadi katika mapenzi ni kuboresha mapenzi. Fahamu kuwa unapompa mpenzi wako
zawadi utamfanya ajihisi kama niwapekee kwako hivyo atajiona kama ni mmoja wapo
kati ya watu wenye thamani kwako na ataamini kama kweli upo karibu yake na
unamjali hivyo hatashindwa kulipa mazuri kwako kwa kukuonesha upendo wa dhati
na utamfanya azidishe mapenzi kwako kwani atakua anajua kuwa wewe unamjali na
unamuonesha upendo sasa kwanini nayeye asikujali?! Hivyo zawadi yako itakuwa ni
njia moja wapo ya kuboresha penzi lako kwa umpendae.
2.
ZAWADI ZINAJENGA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI: Umuhimu wa pili wa zawadi katika mapenzi ni
kujenga taswira ya kumbukumbu kwa mpenzi wako, faham kuwa unapompa mpenzi wako
zawadi inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea
mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako
zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana nawewe kwake
kunatofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako
kwake haitofutika kila azionapo zawadi zako.
Mpenzi msomaji napenda nikushauri juu ya zawadi unazotakiwa kumpa mpenzi wako jitahidi pindi unapohitaji kumnunulia mpenzi wako zawadi tafuta zawadi ambayo itadumu kwa mpenzi wako kama vile nguo, card, maua n.k. Isiwe zawadi ya muda mfupi isiyotunzika kwa mfano unaweza kumpa mpenzi wako hela ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi.
KUMBUKA: sio kwamba usimpe mpenzi
wako hela ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji
na sio katika kuboresha mapenzi.
Zawadi inaboresha
na kudumisha sana penzi jitahidi kutoa zawadi kwa mpenzi wakoo… itasaidia na
haijarishi ni ya aina gani…
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv