baada ya wanasayansi wa neva
wakitumia teknolojia ya kisasa ya kupima ubongo wamegundua kuwa maumivu
mbalimbali yanaweza kuchochea baadhi ya sehemu ubongoni.
Utafiti umebaini mtu
aliyekatika mkono wake katika miaka mingi iliyopita bado anaweza kuhisi maumvi
ya mkono uliokatika, mtu aliyekataliwa na mwingine anahisi maumivu moyoni, na
tunapoona marafiki wamejeruhiwa pia tunahisi maumivu, mambo hayo yote
yanasababishwa na shughuli za sehemu zinazohusiana na maumivu kwenye ubongo
wetu.
Uwezo wa kuhisi
maumivu ya wengine haumilikiwi na binadamu tu. Wanasayansi wamegundua wanyama
wengi wakiwemo panya na sokwe wana uwezo huo pia, ambao unasaidia kuwahimiza
kuwatunza watoto na wenzao kwa makini zaidi na kuongeza uwezo wa kuishi.
Lakini vile vile kuwasaidia
wengine katika mazingira ya asili huenda kukaleta hasara ama hata hatari hivyo
kwa kawaida wanyama wanawasaidia wenzao tu. Binadamu pia wanafanya hivyo,
tunaweza kuhisi zaidi maumivu ya wenzetu, lakini tunapoona wale wasio wenzetu
wamejeruhiwa hatuhisi maumivu.
Utafiti mpya pia
unaonesha kuwa si kama tu panya wanaweza kuona na kusikia maumivu ya wengine,
bali pia wanaweza kuyahisi kwa pua. Watafiti wamegundua kuwa panya mwenye
maumivu anaweza kuwaambia wenzake maumivu yake kupitia harufu maalumu, na wale
wanaohisi harufu hiyo watakuwa rahisi zaidi kuhisi maumivu
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv