Swali : Je, ndoto za mapenzi huathiri vipi
uhusiano?
Jibu ni kwamba inategemea iwapo mhusika
mkuu katika ndoto hizo ni mpenzi wako. Wanasayansi nchini Israeli walifanya
utafiti hivi majuzi Tafiti zinaonyesha
kuwa wanaume huota ndoto za mapenzi zaidi kuliko wanawake, ingawa ndoto hizo ni
kawaida kwa kila mmoja aliye na mchumba au la.
Ndoto za ghafla!
Kila
mtu huota ndoto za mapenzi.
Watu huota ndoto za mapenzi nyakati mbalimbali, si wa ngono peke yake –
wakiwa wamechoka, wanapiga foleni ama kikaonikwa mujibu wa Dkt
Gurit Birnbaum, mwanasaikolojia na mtaalamu wa masuala ya mapenzi katika kituo
cha Interdisciplinary Center (IDC) Herzliya.
Isitoshe, hakuna aliye na udhibiti wa ndoto zote – wakati mwingine
hutokea ghafla,yalisemwa katika kongamano la
kimataifa la utafiti wa mahusiano, 2016 International Association for
Relationship Research (IARR) Conference.
Wanasayansi
walifanya tafiti tatu kuelewa jinsi ndoto za mapenzi huathiri uhusiano wa
wachumba.
Dkt Birnbaum pamoja na
wanasayansi wenzake walifanya tafiti tatu kujaribu kuelewa jinsi ndoto za
mapenzi huathiri uhusiano wa wachumba. Katika utafiti wa kwanza, wahusika
walitakiwa kuota ndoto kuhusu wapenzi wao ama watu wengine. Katika tafiti mbili
zingine zilizosalia, wahusika walitakiwa kuweka shajara ya ndoto zilizowajia
kila siku. Wahusika pia walitakiwa kujibu maswali kila siku kuhusu uhusiano
wao.
Kichocheo cha uhusiano
Ndoto
zaweza kumhusu mpenzi wako ama mtu mwingine.
Iwapo ndoto zako za
mapenzi zinahusu mchumba wako,ni vyema kabisa.
Kwanza, kwa sababu yaonyesha unamtamani mpenzi wako zaidi. Pili,
unathamini mpenzi wako na uchumba wenu na uko tayari kuimarisha mapenzi yenu.
Huu ni uhusiano thabiti,
Iwapo mhusika mkuu
katika ndoto hizo si mchumbako, usihofu.
Kwani Kando na hisia za hatia na aibu, ambazo watu wengine hupata kwa
sababu wako katika uchumba na mtu tofauti na yule kwenye ndoto, hatukupata
madhara mabaya sana. Kwa hivyo jiweke huru, ota ndoto za mapenzi ilmradi hakuna
hatia zozote unazohisi.
Chunga
unachomuambia mpenzi kuhusu ndoto zako kwani zaweza kuyumbisha uhusiano wenu.
Uamuzi wa kumuambia
mchumba ndoto zako za mapenzi ni suala tofauti kabisa.
Uwe mwangalifu sana kuhusu unachomuambia mpenzi wako. Gumzo hiyo yaweza
kuleta uchangamfu na kuboresha uhusiano wenu iwapo mpenzi wako hatahis
kutishiwa na “mchumba” unayemuota. Hivyo, usidondokwe kila kitu ficha mengine.”
Hitimisho Ni
sawa kuota ndoto kuhusu mtu ama kitu unachotaka. Hata hivyo, ukitaka kupata
manufaa ya ndoto za mapenzi itakuwa vyema kumuota mpenzi wako mara moja mbili
hivi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv