Uchunguzi kuhusu
madini na jiografia ya sayari ya Mars unaonesha katika zama za kale sayari hii
ilifanana na dunia tunamoishi na ilikuwa na maji mengi. Lakini swali
linalogonga vichwani mwa wengi ni je, viumbe viliwahi kuishi kwenye sayari ya
Mars? Na vipi hadi sasa bado kuna viumbe vinavyoishi kwenye sayari hiyo yenye
ukame mkubwa? Jibu la maswali haya limepatikana kupitia utafiti mpya uliotolewa
kwenye Gazeti la Nature Communications kwamba ukame mkubwa umekomesha
maisha yote na kuifanya Mars iwe sayari yenye mazingira mabaya kwa viumbe hai.
Katika miaka bilioni 3
iliyopita, Mars ilikuwa na bahari, mito na maziwa na inafaa kwa maisha ya
viumbe lakini sasa imebadilika na kuwa sayari yenye ardhi nyekunduKikundi cha
wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Stirling huko Scottland kimetafiti mazingira
ya hivi sasa ya Mars. Kiongozi wa kikundi hicho Dk. Christian Shroder amesema
hivi sasa ukitaka kutafuta dalili ya viumbe kwenye sayari hii, unatakiwa
kutafuta mapango yenye kina kirefu ambayo yapo mbali na ukame na mionzi.
Kikundi hiki
kimetafiti muda wa madini ya chuma kupata kutu kwenye Mars. Muda huo unahusiana
na kuwepo kwa maji. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa muda huo kwenye Mars ni
mara 10 hadi 10,000 ya muda huo kwenye jangwa lenye ukame mkubwa zaidi katika
dunia yetu. Hii inamaanisha kuwa ukame umeendelea kwa mamilioni ya miaka kwenye
sayari hii.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv