Wanasema msichana/mvulana anayeingia
katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya mapenzi, hukosa umakini
wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa
wazazi wake.
Watu wengi wamejikuta kwenye kashfa za kuitwa
wahuni kwa kubadilisha wanaume/wanawake kwenye maisha yao kwani wataalamu wa
masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha
kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
·kutambua vigezo vya mwenza wako unaye muhitaji;
kwa
kila mwenye mwenza wake inabidi ujue mahitaji ya nafsi yako kwa kujua nini
unataka kwenye mahusiano yako kwani watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu
mahusiano ndo mana unaambulia kuhangaika mara kwa bwana Juma mara kwa hasani au
kwa upande wa wanaume ndo wanabadilisha sketi kam misemo ya vijana wa sikuizi.
·Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za
ndani kivitendo.
Hapa
suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa
hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono.
Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya
kuzingatia.
·Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka;
Lazima
baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao.
Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.
·Ushirikishaji wa ndugu;
Ni
vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo
ni budi yakaendelea au yakasitishwa. mtembezi.com inakushauri usipuuzie
maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini
uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa
pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana.
·kuzungumzia ufanyaji mapenzi,
hapa nina maana kama wapenzi
wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo
na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili
basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.
·kutimiza ahadi ya Ndoa;
kuoana
ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka,
kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya
wengi kutoaminiana.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv