Utongozaji
ni jambo ambalo hutumiwa na kila mtu. Kuna njia kadha wa kadha ambazo zinaweza
kutumiwa kufanya mtu aingie katika mahusiano ya kudumu na yeyote yule.
katika mausiano haijarishi ni mwanaume au mwanamke jukumu la kutongoza liko kwa wote na wanawake waliowengi upenda kutumia ishara na vitendo mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwa wanaume. Na kuna njia kadha wa kadha ambazo mwanamke hutumia kumtongoza mwanaume. Zile ambazo hujulikana sana ni kama:
·
kuangalia macho
·
kumnunulia mwanaume
kinywaji
·
kumsifu
·
kutabasamu
n.k
Hii
ni baadhi ya kutongoza ambako mara nyingi hufanya kazi. Lakini kuna baadhi ya
wanawake ambao hawaridhiki na hatua hizi na hujaribu kutafuta mbinu nyingine
ambazo wanaamini ya kuwa zinaweza kumsahiwishi na kumtia ndani ya 18 mwanaume,
baadhi ya mbinu hizi huwa sawa na nyingine huwa sio sawa .
1. Kuyapanga matiti yako
Hii
inakubalika kutumika kama ni dharura. Kawaida hakukosekani sehemu ya mapumziko
ya mwanamke iwapo anataka kuyatandaza ama kuyatengeneza matiti yake.
Kuyatengeneza
matiti yako yakae vizuri hadharani inaonyesha kukosa ustaarabu na kukosa
heshima kijamii. Si hivyo pekee bali pia wanaume hawavutiwi kamwe na hatua kama
hii. Ukianza kuyatandaza matiti yako huku na kule kunawafanya wanaume kujihisi
kuwa na aibu kimpango.
2. Kuramba midomo yako kiushawishi
Kuramba
midomo yako kwa njia ya kuifanya iingiwe na unyevu inakubalika. Lakini kuramba
midomo yako kana kwamba mwanaume ulietoka naye deti ni ice cream ambayo unataka
kuila inaogofya. Mwanzo kwa mwanamke ukiwa unaramba midomo yako kwa ushawishi
kunaweza kumfanya aongope kuwa unaweza kumla wakati ambapo mtakuwa wawili
pekeenu. Ok, najua kuramba midomo huwa kunaleta hisia za mapenzi lakini haipaswi
kufanywa hivyo sehemu za hadhira.
3. Kuomba msaada wakati ambapo hauhitajiki
Tabia
ambayo wanawake hupenda kuitumia mara
kwa mara, tabia ya kufanya kitu kuwa kina dharura na ambacho anahitaji msaada
wa haraka kutoka kwa mwanaume. Jambo la rahisi analifanya kuonekana zito.Wanaume
wanapenda wanawake ambao wanapenda kujitegemea wao wenyewe, na ambao
hawaonyeshi pupa ya kutaka usaidizi hata kama wanataka.
4. Kurusha nywele kupindukia
Mwanamke
anapaswa kuzirusha nywele zake nyuma wakati ambapo anamtongoza mwanaume lakini
haufai kuzidisha. Kila kitu kina kiasi flani. Hivyo kabla kuzirusha nywele zako
mara kwa mara hakikisha ya kuwa hazitorusha chembechembe yeyote za uchafu ama
kutoa harufu ambayo inaashiria hazijaoshwa kwa muda.
5. Michezo ya kumfinya, kumgonga, kumpiga kofi nk
Kwa
mwanaume, ni vile tu hawapendi kusema kwa nguvu. Lakini ukweli ni kuwa wanaume
hawapendi kuumizwa na kugongwa haswa sehemu za hadharani. Uchungu ni ule ule
hata hauchagui unamuumiza nani. Hivyo tabia kama hiyo haiwapendezi kamwe
wanaume.
6. Kujishika kope zako
Huwa
inaonekana vizuri wakati ambapo unafikiria jambo kama hili, lakini wanaume
wanapoteza umakini wao kwa mwanamke iwapo kila mara atakuwa akizishika kope
zake. Hii ni mbinu ya kutumiwa mara moja na wala si kila wakati. Mara nyingi
itaoneka kwamba kuna kitu kimekuingia machoni mwako, na mwanaume hawezi
kujizuia ila kujaribu kukupuliza ili kusaidia kutoa huo uchafu. Mara nyingi
hatua hii inafanya mwanaume apoteze umakini kwako kwa sababu ya hilo jambo.
7. Kuandama wanaume kila mahali
Wewe
umekuwa mtu mkubwa hivyo tabia za kufuata na kuandama watu kila mahali si
mpango. Unafaa kuacha kuandamana na wanaume kila mahali na uanze kuzungumza
kile ambacho kiko alikini mwako. Fahamu ya kuwa tabia ya kuandamana mtu kila
mahali huwezi kutofautisha iwapo umependezwa ama una tabia za kunyatia.
8. Kula chakula kutoka kwa sahani ya mwanaume
Hii
ni tabia ambayo kuna wanawake ambao wanaipenda sana. Mbona usingojee kama
mwanaume ataagiza kula kwa sahani yake? Kawaida kuna kitu ambacho hakitaonekana
sawa iwapo utarukia kuanza kula katika sahani ya mwanaume. Kama umekuwa ukideti
na mwanaume kwa muda mrefu hio ni sawa. Lakini iwapo umeanza kujuana na mtu
hivi karibuni na kuanza tabia kama hii humchukiza mwanaume hapo hapo.
9. Kujaribu kuongea kuhusu vitu mwanaume anapenda halafu kushindwa
kustahimili
Wanaume
wengi huona ya kuwa inakaa raha iwapo kuna maslahi ambayo anagawa sawa na
mwanamke. Lakini iwapo mwanamke ataiga na kujifanya ya kuwa anagawa interest
moja na mwanaume huwa kawaida atagundulika. Mwanaume anapenda uulize na kujua
vitu anavyopenda. Hawataki uanze kutoa ujuzi na ujanja wote kuhusu jambo fulani
bila wewe mwenyewe kujua chochote ambacho unaongea.
10. Kulalamika kihatia
Wanawake
kulalamika kihatia huwa ni jambo zuri la kuweza kuteka atenshen kutoka kwa
mwanaume, lakini kwa mwanaume anajua hio ni mbinu ambayo mwanamke anaitumia
kama mchezo wa kuichanganya akili yake, Hata kama ulikuwa unataka atenshen
ndogo kutoka kwake, mwanaume ataona kwamba umefanya hivyo maksudi kwa ajili
yao, So tabia kama hio inaweza kuharibu siku yao, na pia wewe iwapo
hawaingiliana na ujanja wako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv