Duniani kuna makundi manne ya watu wanaotafuta
mafanikio, jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wakose majibu ya kwa
nini hawa wafanikiwe kimaisha na wengine wasifanikiwe kabisa.
Katika ulimwengu wa
mafanikio binadamu wamegawanyika katika makundi manne ambayo ni WATENDA USAHIHI, WANAOLIDHIKA, WANAOTAKA KUPENDWA
NA WASHINDI.
WATENDA USAHIHI:
Hawa ni watu ambao
katika maisha yao huwa hawataki kukosea au kuonekana wayafanyayo si sahihi.
Watu wa aina hii huwa ni wagumu sana kufanya jambo ambalo akili zao hazihakiki
kuwa litamalizika kwa mafanikio.na Kikwazo kikubwa kwa watu wa aina hii mara
nyingi ni kusitasita katika kuamuzi. Ni watu wa kuogopa macho ya watu hasa
suala la kushindwa kutimiza malengo linapowajia akilini. Kinachowaogopesha
zaidi watu wa kundi hili ni kuaibika mbele za watu jambo fulani
likiwaharibikia.
WANAOLIDHIKA:
Kundi jingine la
watu katika ulimwengu wa mafanikio ni wale wanaolidhishwa na hali zao na kwamba
hawahitaji mabadiliko ya aina yoyote kwenye maisha yao. Hata hivyo, wapo
wanaozoea kazi na majukumu yao ya kila siku kiasi kwamba hawataki kubadilika,
hawapendi kuongezeka zaidi ya hapo walipo. Utakuta uwezo wa mfanyakazi alioanza
nao miaka 7 iliyopita ni huohuo mpaka leo.
Wafanyakazi wengine
wanaweza kuajiriliwa nyuma yake wakajitahidi kusoma, kujifunza kazi na kupanda
vyeo na kumwacha mlidhikaji yuko palepale. Kundi la wanaolidhika.
WANAOTAKA KUPENDWA:
Kuna watu katika
maisha yao wanataka kumfurahisha kila mtu kwa lengo la kuvuta upendo wa
wanadamu wenzao. Asilimia kubwa ya kipato chao hukitumia kwa lengo la
kuwatumikia ndugu na marafiki, kuwasaidia katika shida zao na kujikuta wakisahau
kufanya mambo yao ya kimaendeleo.
WASHINDI:
Kundi la mwisho la
watu ni wale ambao katika maisha yao ya kila siku hupenda kufika kwenye kilele
cha mambo yote wanayofanya.
Hutamani kufanikiwa
zaidi na zaidi, hawakubali jambo liwashinde, kila walichokusudia kukifanya
huakikisha kwamba wanakabiliana na changamoto zote na mwisho wa safari kupata
ushindi.
Jiulize; Je ni sahihi kutokuwa makini katika mambo yako ama
kulidhika na mafanikio uliyoyapata? Je ni
sahihi mtu kuacha kuwasadia wenzake kwa hofu ya kuwa katika kundi la tatu?
Jibu ni hili: Ni vema mambo matatu ya mwanzo yakaongozwa na la
nne yaani USHINDI. Kwa
maana hiyo kila mmoja wetu lazima awe mtu ambaye anatamani sana kufanikiwa
katika maisha yake ya kila siku.
Watu wote wakiwa na
nia hii wataweza kuyapita makundi mengine matatu kwa uangalizi mkubwa. Hawatakubali
wawe makini wasifikie malengo, hawataacha kujaribu bahati kwenye mambo ambayo
akili zinaona ni magumu, hawatalidhishwa na mafanikio au hali walizonazo na
hawatakubali kutumika kama wafurahisha watu bali kwa kila kitu watafanya kwa
kiasi kwa lengo la kufika katika mafanikio sahihi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv