Inashauliwa sana Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh.
Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake.
Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt). Razi amesema Kitunguu maji kikifanyiwa achari, ukali wake hupungua na hutia nguvu maida, na kitunguu kilichofanywa achari, hufungua mno hamu ya kula Kwa ajili hiyo watu wa misri hula ktunguumaji kikiwa kimechomwa, hutia nguvu mwilini, huufanya uso kuwa mwekundu na huimarisha misuli
Ibn Baitar anasema Kitunguu maji hufungua hamu ya kula, hulainisha tumbo. Kikipikwa hukojoza na huzidisha nguvu za kiume kikichemshwa. Na kinachokata harufu ya kitunguumaji ni lozi (almond).
Al-Antaky amesema kuhusu kitunguu maji kwamba Hufungua vizuizi mwilini, hutia nguvu za shahawa kwa mwanamke na mwanaume mbili (ya kula na na kujamiiana) hasa kikipikwa kwa nyama, pia huondoa homa manjano (jaundice) hukojoza na kumimina hedhi pamoja na kuvunja vijiwe tumboni.

Pia imethibitishwa kuwa katika kitunguu maji kuna vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwahivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea) na huua aina ya vijidudu vingi vya hatari. 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top