Napenda kusisitiza kuwa miguu ni sehemu ambayo inatakiwa
kutunzwa kwa upekee kama ilivyo sehemu nyingine ya mwili kama uso, haijlishi
miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa
utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.
Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako
hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa. fanya hivi:
Chukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni
maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa
robo saa hivi.
Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paka
na ikikauka anza kusugua miguu yako hadi kwenye vidole na unyayo, kisha
jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.
Pia unaweza kutumia baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili
kuitengeneza miguu yako na vinapatikana kwenye maduka yote ya vipodozi na hapo
usikurupuke ulizia kwa wataalamu ili upate maelezo ya jinsi ya kuvitumia.
Pia unaweza kutembelea baadhi ya saluni ambazo zinatoa huduma
hiyo jitahidi hata mara moja kwa mwezi kuhakikisha miguu yako inapata huduma
nzuri ili iwe ya kuvutia.
Kwa wale ambao miguu yao ni makovu au madoadoa wajaribu kutumia
scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa kutumia
cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani zinasaidia sana kuondoa
madoa.
Pia unaweza kuchukua ukwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika
changanya mchanganyiko huo na asali kisha paka kwani husaidia kuondoa madoa
kwenye miguu.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv