Vijana na wanaume huwa wanaambizana kwamba ili uhusiano udumu, usimueleze kila kitu mwanamke. Wanasema mfiche asijue kila kitu.
na Taswira hiyo pengine kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, sasa inakuwa kama sheria. Wanaume wanasambaziana mbinu hiyo ili kukabiliana na wanawake zao. Wanaona ni bora kuwaficha baadhi mambo ili mambo yaende vizuri.
Mwanaume anaamini akimficha baadhi ya vitu mkewe, inasaidia kumfanya aishi kwa amani. Hataki kumueleza kila kitu kinachomhusu kwani anaamini uwezo wake wa kukabiliana na mambo hauwezi kuwa sawa na yeye hivyo bora amfiche.
Hali hiyo haikuja hivihivi, imetokana na visa mbalimbali wanavyokutana navyo katika uhusiano. Wanafikia hatua ya kuwafananisha wanawake na watoto. Kwamba hata kama mwanaume hana fedha, hapaswi kumueleza mwanamke kuwa hana fedha.
Kwamba mwanamke usimueleze vyanzo vyote vya mapato maana ukimueleza ni tatizo. Lazima ataleta usumbufu. Atakuwa wa kwanza kuhoji matumizi na
kutaka kila kitu wapange wao.
Mwanaume asipokubaliana naye, anakuwa wa kwanza kuleta chokochoko ambazo mwisho wa siku zinasababisha mtafaruku ndani ya nyumba. Hapo ndipo wanaume wengi wanapopakwepa.

Hivyo wanaume wanakubali kuumia kimoyomoyo. Hamuelezi hata siku moja ukweli kuhusu mapato yake. Hata kama hana kitu, mkewe au mchumba wake akiomba fedha, anampa tu matumaini kwamba asiwe na wasiwasi atampatia siku fulani hata kama hana uhakika wa kuzipata. 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top