Karibu sana msomaji wa
edonetz katika makala za kila siku na leo tuzungumzie kumpenda aliyependwa, Kupenda hakuna
macho! Moyo ukishapenda hausikii wala kuambiwa. Katika hili ndiyo maana
unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa
lakini moyo wake ndio umeshapenda.
Hayo ndiyo mapenzi
jamani!, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari
ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu
sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Kuna mambo kadhaa ya
kukusaidia kama yafuatayoo
Kwanza… Chunguza
Tumia muda wako mwingi
kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni
watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo
uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future
naye.
Pili… Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza,
ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘serious’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha
moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea
kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Tatu… Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda
msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya
moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni
mtu anayeonesha kukumisi
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Nne… Ni rahisi kubadili
uamuzi wake?
Unadhani huyo
uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye
kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza
kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
Tano… Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane
na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na
demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv