Viumbe hai kwa ujumla
tunasifa ya kupumua kupitia mifumo mbalimbali ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka
katika miili yetu,kupumua huku si tu kunatufanya kutimiza moja ya kazi na sifa
ya mwili bali pia huwa ni kama tiba kwa upande mwingine.
Kujisaidia haja kubwa
na ndogo lakini kupumua kwa kutoa hewa kupitia kinywa,makalio(kujamba) na vinyweleo katika ngozi
Kujamba inaweza kuwa
kitendo cha aibu kwa wengi wetu, inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni
tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.Kila mtu anajamba,
Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa
na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni
hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.Hewa ingine husababishwa na gesi
kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na
kemikali katika utumbo au bakteria.
Kwa kawaida “ushuzi”
unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni
carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.
Asilimia moja tu ya “ushuzi” inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina
sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya “ushuzi” utoe harufu mbaya
Kujamba huambatana na
sauti,hii ni kutokana na “vibration” katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio
wa kujamba hutegemea “presha” inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli
ya njia ya haja kubwa.
Kwa nini Ushuzi hutoa
Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi
hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha
hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage,kabichi,soda na mayai.
Watu hujamba hadi mara 14
kwa siku.
Mtu wa kawaida hutoa
hata nusu lita ya ushuzi kwa siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa
kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la
atomiki.
Ushuzi husafiri kwa mwendo
wa futi 10 kwa sekunde.
Harufu ya ushuzi
huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua
muda mrefu kwa harufu kufikia pua.
Kujizuia Kujamba Inaweza
Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari
hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya
wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng’enyo wa
chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.
Wengine wanadhani
kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi,na pia inaweza
sababisha bawasili (hemorrhoids).
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv