Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi.
Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili
linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika
matumizi ya neno hili
Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha
moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda
kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi. Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika
nakuonekana unajali.
Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja
kwa kosa moja ndo mana wanasema, kosa sio kosa ila ukirudia
kosa ndio kosa. Kama ulikua
haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika
matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua
ulizozifanya.
Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila…….
Siamini kama haya yangetoa………
aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha
ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest
forgiviness .Utapelekea upande wa pili uliokosewa kukuamini tena
na ni rahisi kusamehe na kusahau tofauti na kuwa na maneno
meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa.
Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa
upesi
- Kubali
kosa pale ambapo umetenda,NOTE;
Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au
hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa
- Badili
mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa
- Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe)
- Usilazimishe
kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano
kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu
sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea
na jinsi mlivyo
- Anayeomba
msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika
kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila wanakukumbuka,
endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa
huwa ni mtu wakusema; hiyo ni kawaida yako ina maana anashikilia vitu
moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na
tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye
atakukosea.
- JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOWfb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv