Watafiti
wa masuala ya kimapenzi tunaamini kwamba, mvuto wa mapenzi miongoni mwa
wapendanao hupungua kadiri siku za uhusiano wao zinapokuwa nyingi, ushahidi
unapatika kwa takwimu za usaliti kuwa chini ya 13% kwa mapenzi yenye
muda wa kuanzia mwezi mpaka mwaka mmoja. Inabainishwa kuwa kiwango cha watu
kusalitiana hupanda sambamba na umri wa uhusiano wenyewe. Lakini upo ushahidi
wa wengi kuanza kurejesha uhusiano waliokufa, pindi wanapoishi na wenza wao kwa
muda mrefu kiasi cha kuzoeana sana.
Hali
hii hutokana na kukinaishwa na penzi la wapenzi wao na hivyo kuhitaji mshawasha
mpya. Kushuka kwa msisimko wa kimapenzi kuna dalili nyingi lakini kubwa kati ya
hizo ambayo ndiyo huwasumbua wengi hasa wanaume ni kushindwa kufanya tendo la
ndoa na wenza wao au kutenda na kupata starehe chini ya kiwango.
Jambo
kubwa katika tatizo hili ni matokeo baada ya watu kupatwa na hali ya kupoteza
hisia za mapenzi. Wengi wao wamekuwa wakiamua kuachana na wenza wao na
kuanzisha uhusiano mpya kwa msukumo wa hisia kali za mapenzi machanga ambazo
walikuwa nazo hata walipokutana na wale wanaoachana nao.
Kitalaamu
ukitafsiri uamuzi huo, unapata kasoro za ufahamu ambazo zinahitaji elimu. Watu
wengi wamekuwa wakiuliza, wanaweza kufufua penzi lililokinai? Jibu ni kwamba WANAWEZA, endapo watafuata mambo yafuatayo kwa vitendo.
JAMBO LA KWANZA ni kujenga ufamilia
na umpendaye, nikiwa na maana kwamba awe rafiki na mtu wako wa karibu katika
matembezi na maongezi. Wengi tunakutana na wenza wetu wakati wa kulala, sasa
huo msisimko wa kimapenzi utapatikana wapi katika mazingira haya?
JAMBO LA PILI, ni kumthaminisha mwenza wako kwa ubora kila wakati. Msisimko wa kimapenzi hauweza kuja kama hujavuta hisia juu ya jambo au maumbile fulani ya mwenza wako. Inashauriwa kila mara umtazame mpenzi wako kwa kumtathimini vema na kujivunia, miguu yake ya bia, umbo namba nane, kasheshe zake faragha na mvuto wake kwa ujumla. Ukiwa na vitu hivi vitakusaidia katika kuzalisha homoni na kukuza hisia zako.
JAMBO LA TATU ni kuwa na kitu kinachoitwa uchumi wa kimapenzi ambao hutokana na kumfikiria mpenzi wako kila mara unapokuwa kazini, kwenye matembezi na ikiwa unaona vitu barabarani au kwenye maduka jaribu kuwaza au kuvinunua kwa ajili ya kukuza penzi lako. Hapo utafanikiwa kukuza penzi.
JAMBO LA NNE ni kuazima hisia. Kwa mfano unaweza usiwe na msisimko na mpenzi wako lakini ukawaza mwanaume mwingine na kumfananisha na uliyenaye, hili si jambo baya na linatajwa kusaidia kuamsha penzi lililokinai. Kama hilo halitoshi kuazima hisia kunakwenda mbali hadi kwenye kupokea sifa toka kwa rafiki zako zinazomhusu mwenzako, mfano. “Mume wako mpole anavutia kweli” Kauli hizi ukizitafakari zitakusaidia kufufua mapenzi yako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv