Unaweza kumfanya mwanao awe smart kwa chakula tu! kuna vyakula vinarutubisha ubongo kuliko vingine,  sasa ukivikazania hivyo utakuta mwanao anakua smart kuliko wengine wasiokula vyakula hivyo.

Siri iko kwenye kifungua kinywa!
wataalam wanasema kazi yake si kufungua kinywa tu, hata ubongo unafunguka. Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanaopata kifungua kinywa wanafanya vizuri kwenye test za kuangalia attention na kumbukumbu, kuliko wale wasiopata kifungua kinywa. Na wote tunajua, attention ya darasani ndio inamfanya mtoto aelewe, kumbukumbu ndio inamfanya afanye vizuri kwenye mtihani au hata application ya vitu alivyojifunza baadae. So bila hivyo vitu viwili mtoto kufanya vizuri darasani si rahisi.

Kwa nini kifungua kinywa?

Kwa sababu chakula ndio mafuta ya miili yetu, sasa mtoto anaamka mafuta yamepungua, inabidi ajaze tank lake
(tumbo) ili kila kitu kiende sawa, including brain yake.
Ila sio kila chakula kina matokeo sawa. Lakini kitu chochote ni kizuri zaidi ya kingine, maana watoto wengine wanachagua sana vyakula.

Baadhi ya vyakula vya kurutubisha ubongo:


Peanut butter (siku hizi zinapatikana sana, mini market yeyote unapata)
Mayai
Ndizi mbivu
Maziwa
Mtindi

Asali (unaweza kuipaka kwenye mkate)
 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top