Kipindi
cha kujifungua wengi hutabiriwa lakini siku rasmi mara nyingi haitabiriki. Wengi
hufikiria kuwa dalili ya kwanza ya kutaka kujifungua ni kupasuka kwa chupa. Hii
si sahihi, chupa inaweza isipasuke hadi hadi hatua za mwisho.
Mara
nyingine hulazimika kuipasua ili kuharakisha hatua za kujifungua. Dalili za
wazi kabisa za kujifungua ni ile ya kuwepo kwa uchungu ambazo asili yake ni
katika mfuko wa uzazi.
Uchungu
huu ni ule ambao una mpangilio na ongezeko kwa muda maalumu ambao huenda
sambamba na kusinyaa na kufunguka kwa shingo ya mfuko wa uzazi.
Dalili
ya kufunguka huku huwa ni kutokwa kwa ute mithili ya mlenda uliochanyika na
damu. Ni lazima kwa mjamzito anapopata dalili hizi kati ya wiki 24 na 42
kuripoti katika kituo cha afya ili achunguzwe.
Hata
kama hali hii ikitokea kabla ya muda huo, ni lazima kuwahi kwemye kituo cha
afya kwani ni dalili ya mimba kutoka.
Dalili
nyingine inayoashiria kujifungua ni kushuka kwa mtoto kwenye nyonga katika
mwelekeo wa kutoka kupitia njia ya uzazi. Jambo hili lazima liwepo baada ya
uchungu na kufunguka kwa njia.
Kama
uchungu na kufunguka kwa njia vinakuwapo lakini mtoto hashuki wala husogea
kwenye njia za kutokea, basi lazima huchukua hatua za kujua sababu.
Kukwama huku kunaweza kuletwa na sababu nyingi. Moja ya sababu hizo ni
kutokuwapo kwa uwiano mzuri kati ya ukubwa wa kichwa cha mtoto na ukubwa wa
nyonga ya mama.
Kwa
kawaida kama mjamzito anaendelea vizuri na hakuna vikwazo, huchukua wastani wa
saa nane mpaka 12 kujifungua. Muda huu huwa zaidi ya hapo kama mtoto amekwama
kwa sababu yoyote ile.
Mtoto
aliyekwama huwa katika hatari ya kupoteza maisha kama hatua za haraka hazita
chukuliwa. Inapopaswa kueleweka kwamba kitendo cha kujifungua ni hatarishi
wakati wote na hivyo uangalizi na ufuatiliaji wa kila hatua muhimu.
Wakati
mwingine dharura inaweza kutokea wakati wowote na kulazimika kufanywa uamzi
ambao hapo awali hakufikiriwa.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv