Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza
kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo na Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini
yalipoanza na hayakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye
maeneo machache.
Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania
serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967,
kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea
kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.
Tangu kipindi hicho nchi yetu ya Tanzania iliweza
kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa
dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila
Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.
Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo
kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26
mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.
Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg
Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.
Enzi
za uhai wake, Theresa alikuwa akiishi
peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia
nyumba hiyo Mtanzania aitwaye Othman Lukindo.
Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja
na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na
kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.
Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa
akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger
ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.
Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na
kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini
ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.
Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali
zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za
magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.
Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi
kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya
muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo).
Mkoa
wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.
Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata
warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi
kufikia hatua ya kushiriki shindano la ‘Miss Tanzania’.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na
youtube@edone tv