Watu wengi
hupumbazwa na furaha ya kupata ofa ya kazi waliyokua wanataka, kiasi cha
kuwasababishia kukubali masharti yanayokuja na ofa bila kuyaafiki.
“Huwezi kupata malipo
unayostahili bila kujadili mshahara.”
Unatakiwa
ukumbuke kupata ofa ya kazi sio mwisho wa mahojiano na badala yake unaingia
kwenye sehemu ngumu zaidi ambayo ni makubaliano kuhusu malipo ya mshahara na
marupurupu mengine.
Unaweza kuwaza
kwamba labda mwajiri wako atabadili mawazo ukiomba fedha zaidi, au usubiri
mpaka uthibitishe uwezo wako ndio uombe mshahara unaotaka.
Lakini kupata
mshahara unaotaka, kunategemea kwa kiwango kikubwa na jinsi unavyojiamini. Kama
unajua ujuzi utakaoleta kwenye kampuni na thamani yake, lazima uwasilishe
pendekezo zuri kuhusu malipo yako.
Hata
hivyo, zaidi ya kujiamini kuna njia unazoweza kutumia kuafikiana mshahara baada
ya kupata ofa ya kazi.
Fanya utafiti katika sekta
Kufanya utafiti
wa kiwango cha mshahara kilichopo kwenye sekta ya kazi unayoomba, ni suala
muhimu kabla ya kwenda kufanya usaili wa kazi. Hii ni kwa sababu waajiri wengi
watakuuliza kuhusu mshahara unaotegemea kulipwa.
Uliza kwa jamaa
na marafiki au fanya utafiti mtandaoni na ukishajua kiwango, ongeza asilimia 30
ili upate nafasi ya kufanya maelewano na wahusika.
Jadili bima, mifuko ya jamii
na faida nyingine. Ukishapata ofa ya kazi mwajiri wako atakupa mgawanyo wa mshahara wako,
michango na bonasi. Akishafanya hivi sasa ni zamu yako kuleta mahitaji yako,
usianze na mshahara au bonasi badala yake uliza maswali kama mchango wako
katika mfuko wa jamii. Asilimia ngapi ya mshahara itatumika na mwajiri atachangia
kiasi gani. Aina ya bima ya afya, gharama yake na kama utarudishiwa gharama za
usafiri kwenda kwenye mikutano ya kikazi.
Useme hivi wakati wa maafikiano ya
mshahara?
Kusaidia
kufikisha maombi yako kwa urahisi, unaweza kusema kitu kama; “Nina furaha ya
dhati kuanza kufanya kazi na nyinyi, Ninaamini nitaleta mchango na mafanikio
makubwa hapa. Nimetathmini ofa yenu ya Sh2,000,000 lakini kutokana na uzoefu
wangu wa miaka mitano katika sekta hii na wateja ambao nitawaleta hapa, nilikua
nategemea ofa ya Sh3,500,000.’’
Kumbuka mwajiri
wako anategemea majadiliano haya, hivyo kistaaarabu sisitiza kuhusu mshahara
uliokuwa unategemea. Atakapokupa jibu kwamba hawezi kuongeza mshahara na
ukajiridhisha kwamba hawezi, omba muda wa kufikiria.
Usisahau kuhusu bonasi
Ukiondoa
mshahara, unaweza pia kujadiliana na mwajiri kuhusu bonasi. Tumia utaratibu
kama uliotumia wakati mnaelewana kuhusu mshahara. Hapa kumbuka kuuliza bonasi
yako itakokotolewa vipi? Nani atakuwa na wajibu wa kutathmini na kuamua bonasi
yako na utaipata kila baada ya muda gani?
Usipouliza hutojua
Watanzania ni
watu wastaarabu, wengi tunaona aibu kuongelea ni fedha kiasi gani tunahisi
tunafaa kulipwa. Lakini hakuna ambaye atakataa kulipwa zaidi ya anacholipwa
sasa.
Kwa hiyo, njia
bora ya kupata fedha zaidi kutoka kwa mwajiri wako ni kumwambia kiasi
unachotamani kutokana na majukumu anayotarajia kukupa.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv