Hakuna ajuaye siku wala saa Kifo kitakapotokea ni
fumbo kubwa katika maisha ya mwanadamu. ila Wapo mastaa ambao enzi za uhai
wao walijikuta wakiimba au kufanya mambo yenye kuashiria
kuwa walikiona kifo chao na kwamba wanakaribia kupatwa na umauti.
Hii ni orodha ya mastaa mbalimbali wa
hapa nchini na nje ya nchi ambao wamefariki dunia muda mfupi au siku
chache baada ya kufanya kazi zilizozungumzia kifo au maisha baada ya kifo.
STEVEN KANUMBA
Huyu alikuwa ndiye
kinara wa filamu Bongo lakini kabla ya mauti kumfika 2012, alipata kutoa
kazi yake iliyoitwa Ndoa
Yangu ambayo simulizi
yake ni kama alijitabiria kifo chake, licha ya filamu hiyo Kanumba ambaye
alifariki baada ya kudondoka chumbani kwake, aliimba wimbo uitwao Nitayainua
Macho Yangu ambao ulichezwa
na redio nyingi baada ya kifo chake, ulikuwa ukizungumzia maisha baada
ya kuondoka duniani.
ANGELA CHIBALONZA
Mwanamama huyu ambaye
ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), aliyeishi na familia
yake jijini Nairobi nchini Kenya, alifariki kwa ajali ya gari katika
Barabara ya Naivasha. Kabla ya kufikwa na umauti, mwimbaji huyu alikuwa
amekwishatoa nyimbo nyingi ikiwemo ile inayozungumzia maisha ya peponi
ambayo inakwenda kwa jina la Kutoka Chini.
FANUEL SEDEKIA
Mwimbaji huyu wa
nyimbo za Injili alifariki dunia mwaka 2009 katika Hospitali ya Poriya
Tiberia iliyopo nchini Israel baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa
kisukari. Alikuwa amekwenda huko kwa ajili ya maombi. Siku chache kabla ya
kifo chake mwanamuziki huyu alitoa wimbo uliokwenda kwa jina la Safari
ya Imani ambayo ndani
yake kuna maneno yanayoelezea safari ya kuelekea peponi.
JOHN KOMANYA
Mchungaji huyu wa
Kanisa la Cathedral of Joy International Tanzania, ambaye alikuwa pia ni
mwimbaji wa nyimbo za Injili alifariki dunia mwaka 2015 katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na
tatizo la mishipa inayopeleka oksijeni kwenye ubongo kufeli. Kabla ya
kupatwa na umauti, Komanya aliimba Wimbo wa Bwana
Niinue ambao pia
unazungumzia maisha baada ya kifo hali ambayo ilichukuliwa kama alikiona
kifo chake.
GATARE EPHRAIM, AMOS
PHARASI, PHILBERT MANZI
Hawa ni wanamuziki
watatu wa kundi maarufu la Kwaya nchini Rwanda la Ambassadors Of Christ
ambao walifariki baada ya kupata ajali ya gari. Kabla ya hapo, kundi hilo
liliimba wimbo maarufu wa Kwetu Pazuri ambao unazungumzia maisha ya mbinguni.
Zipo simulizi
zinazosema, wakiwa njiani, Gatare aliyekuwa kiongozi, aliwaambia wenzake, “Nyote mlio katika gari hili, lazima mjue
kila mtu ana jukumu la kuongoza kundi hili hata kama kesho mimi
sitakuwepo”
wakati Amos naye alisema “Kazi niliyotumwa kufanya katika kundi hili nimemaliza, imebaki kwenu kuiendeleza.”
wakati Amos naye alisema “Kazi niliyotumwa kufanya katika kundi hili nimemaliza, imebaki kwenu kuiendeleza.”
Naye Philbert alisema “dada nakuomba msamaha, hata kama wewe
ndo umenikosea, nami jinsi nilivyopokea, naweza kuwa nimekukosea pia.” Dakika kumi baada ya kauli hizo, gari lililowabeba wanakwaya
hao liligongana na lori katika Kijiji cha Tinde, Kahama mkoani
Shinyanga na watatu hao walifariki dunia hapohapo.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv