Ubunifu
ni suala la kujifunza, baadhi ya
wanaume waliokuzwa kwenye jamii yenye mfumo dume (Waafrika kwa ujumla)
huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, “kupenda
kwa vitendo” huenda sio kwamba hataki bali hajui.
Kwa
maana hiyo sio mbaya tujifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye
furaha kwa kufuata haya mambo machache ambayo wanawake wengi huwa
hupenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na vitendo.
…Hakuna kitu wanawake
wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa
busu mara kwa mara.Kabla
hujakurupuka kitandani hakikisha umemkumbatia na kumbusu hata kama kalala
(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).
…Mwambie jinsi gani unampenda na
unavyopenda chapati, mayai, viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo
wa asubuhi.
…Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu
ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo
cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje baada ya kupata
kifungua kinywa.
…Onesha unajali kwa kumjulia
hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako
na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako
pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali
unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani.
…Ufikapo nyumbani mkumbatie
na busu la mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili
huko utokako.
…Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, Wazaramo hununuliwa khanga au hereni na mikufu
ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti,
kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kesi;
mwanamama anafurahi kwelikweli sasa wewe fanya kile unachomudu sio kila
siku wala kila mwezi.
…Msaidie kusafisha meza au jamvi mara baada ya mlo wa
jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani
‘mna-share’ kufanya usafi ili kuokoa muda.
Lolote litakalotokea kila
la kheri, lakini hakikisha unambusu na kumkumbatia kabla hujaanza
kukoroma.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv