Katika
kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa
kawaida wanawake hupoteza kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini mwilini. Hivyo Hali hiyo huweza kusababisha upungufu
wa damu kama mwanamke atakuwa hapati lishe bora na ya kutosha.
Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na madini
mwilini, msichana anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na chokaa kwa
wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-
Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa
1. Mboga za majani
2. Maharage
3. Soya
4. Samaki
5. Maziwa
6. Korosho
7. Mayai
8. Zabibu (Juisi yake)
9. Matunda damu
10. Dagaa n.k.
Mbali na vyakula
hivyo, pia mwanamke huhitaji kunywa
maji ya kutosha kipindi hiki na
kuzingatia hali ya usafi wa mwili, hasa sehemu za siri .Unatakiwa kutumia
vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya
usafi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv