Neno moja la msingi sana kwa vijana naweza kuwapa, ni kutambua nguvu kubwa waliyonayo watoto wa kike, katika mahusiano.
Ni wazi kabisa kuwa mwanamke huna nguvu za mwili za kuweza kupambana au kufanya kazi kama wanazofanya vijana wa kiume, lakini unayo nguvu inayozidi tani hata elfu moja ya mawe. Nguvu ya mwanamke iko kwenye uanamke wake, lakini uzuri wa umbo, elimu, sura, sauti na hata mwendo ni nyongeza nyingine inayokuongezea nguvu hizo. Kwa ajili hiyo, ni makosa makubwa kuona mtoto wa kike anapata tabu katika maisha yake, anakosa anachohitaji au anashindwa kufikia malengo yake.
Nguvu za mwanamke zipo katika kushawishi, kwa maneno na hata vitendo, achilia mbali hisia. Kuna jambo moja linalosababisha watoto wa kike wanakosa uwezo wa kutumia nguvu walizonazo kwa ajili ya maisha yao, kukosa nidhamu.
Wadada wengi na akina mama wanakosa nidhamu katika maisha yao, kitu kinachosababisha wanapoteza nguvu zao na hivyo kugeuka kuwa dhalili.
Nidhamu inayozumgumziwa ni ile ya maisha yao binafsi. Mtoto wa kike unapaswa kujiheshimu kwanza wewe mwenyewe, unapaswa kuuogopa mwili wako usigusweguswe ovyo na wanaume, uupende. Hata kama huna uwezo wa kusuka nywele saluni, unaweza kubaki na ubora wako. Mwanamke anayejiheshimu, anawatisha wanaume.
Na nikwambie kitu ,Namna mwanamke anavyojiweka, ndivyo mwanaume anavyomchukulia. Ukiwa mtu rahisirahisi, nao wanakuja kirahisirahisi, ukiwa makini, unawapa wakati mgumu sana kukusogelea, maana hawana uhakika kama watakupata au la.hakuna kitu kinawauma wanaume kama kukataliwa, ni bora akae kimya asikutongoze kuliko atupe ndoana zake halafu akukose.
Kwa hiyo ili uweze kuonyesha nguvu yako, ni lazima ujiheshimu. Ukijiheshimu, mwanaume atakayekuja, atakuwa anajiamini. Na katika mazungumzo ukimuelewa, basi unaweza mwambia unachotaka, kwa mfano siwezi kujiingiza katika mapenzi sasa hivi, natafuta kazi kwanza ili niweze kumsaidia mama yangu.
Mwanaume anaweza kujiingiza mwenyewe kuwa atakutafutia kazi na mama yako atamsaidia. Vivyo hivyo pia kama unataka kujiendeleza kielimu na vitu vingine. Lakini kama wewe kazi yako ni mwepesi, mwenye kutaka hela tu kila siku, watakuchukulia hivyo hivyo, wanakupa hela, wanapata wanachotaka halafu wanakuacha! na kuondoka zao.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz_blog , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv