hivi unajua jinsi ya kupunguza mwili kwa njia rahisi kabisa ya kutumia maji. Wengi tunaijua njia ya kunywa maji glasi nane kwa siku lakini hii ni njia mpya kabisa ambayo ukiitumia itakupa matokeo ndani ya kipindi kifupi. Kabla ya kuifanyia kazi njia hii, hakikisha unapima kwanza uzito wa mwili, baada ya hapo anza kuitumia.
MAJI GLASI 2 KILA MLO Wataalamu wa afya huwa wanakataza kunywa maji wakati wa kula, wengi hudai kuwa si sawa kwa afya lakini hapa unatakiwa kunywa glasi mbili kabla hujala. Asubuhi kabla hujanywa chai, kunywa maji hayo. Ikifika mchana pia kabla ya kula, kunywa maji glasi mbili.Usiku fanya hivyo hivyo.
MUHIMU Kila baada ya wiki hakikisha unapima uzito na utaona matokeo. Kumbuka hata kama utakuwa unafanya hii ‘diet’ ya maji, punguza vyakula vya sukari, mafuta na ulaji wako uwe wa kipimo.
KUMBUKA NA ZINGATIA
Ukinywa maji kabla ya chakula itakusaidia usile sana. Hata kama ulikuwa umepania kula kivipi, utakula kidogo kisha utakuwa umeshiba. Pia maji yatasaidia kusaga chakula tumboni.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz_blog , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv