Jaman najua kuachana na wapenzi wa kwanza huumiza, wakati mwingine inawapelekea watu kuwa watumwa wa mapenzi na inakuwa vigumu kupona vidonda vyake na wengi huyumba sana kimahusiano wanapopata wapenzi wapya.

sasa leo tuangalie hizi baadhi ya hatua za kuchukua ili umsahau mpenzi wako wa kwanza, usonga mbele;

... Kata mawasiliano, hakikisha hakuna mawasiliano ya aina yoyote iwe ni simu, fb, au outings na ex wako
... Kumbuka ulichokichukia sana kwa ex wako, yote mabaya au mapungufu yake yatakufanya uone umetua mzigo mzito katika maisha yako.
... Amini kuwa kila kitu hutokea kwa mpango wa Mungu na kuwa atakuwa amekupangia kizuri zaidi ya ulichokipoteza
... Uwe wazi, zungumza na marafiki na ndugu kupunguza msongo wa mawazo.
... Punguza au acha kabisa kutumia zawadi zake; nguo, saa au vitu vinavyoweza amsha kumbukumbu yake.
... Omba sana Mungu ukijua kila kitu kitapita isipokuwa yeye aliye juu ya vyote, atakupa aliyekupangia.

Lakini pia ningependa kukushauri usikurupuke kuingia ktk mapenzi mapya au kusema unaziba nafasi yake ni vizuri kwanza utulize akili yako na mawazo yasahau kabisa kuhusu mapenzi hii itakusaidia sana kumpata alie bora zaidi ya yule uliemuacha..

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz_blog  , inst@edonetz_blog na  youtube@edone tv
 
Top