Image result for viazi
Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani.
Hii ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema.
Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000.
Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga
Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari.
Image result for wajawazito
Kubadilisha ulaji huu wa viazi (chips) kwa wiki kwa kula mboga mboga nyingine kunaweza kuzuia hatari hii, wanaeleza waandishi wa utafiti huu.
Wataalam wa masuala ya lishe nchini Uingereza wanasema vyakula vyenye wanga ama vya kuongeza nguvu na joto mwilini kama vile viazi, vinapaswa kuwa theluthi moja ya vyakula vinavyoliwa na watu.
Utafiti huo unatarajia kuchunguza nini chanzo cha maradhi ya kisukari yanayowapata baadhi ya wanawake wawapo wajawazito .
Utafiti huu umefuatia wauguzi wawili waliopata ujauzito kati ya mwaka 1991 na 2001. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuwa na maradhi ya kudumu kabla ya ujauzito.

 Source…Bbc.IUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top