Kwa mujibu wa utafiti mbalimbali, maharage, hasa
meusi ni chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya faiba kinachoshusha kiwango cha
kolestro mwilini. Vilevile kiwango cha faiba kilichomo kwenye maharage meusi,
huweza kudhibiti kiwango cha sukari kisipande haraka baada ya chakula, hivyo
kufanya maharage kuwa lishe nzuri kwa wagonjwa wa kisukari na shinikizo la juu
la damu.
Iwapo utapata mchanganyiko wa maharage meusi na
ule mchele ‘mweusi’ ambao haujakobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu
brown rice, basi utaweza kupata kiasi kikubwa cha protini na faiba ambacho
huwezi kupata kutoka katika chakula kingine.
Utafiti wa muda mrefu uliofanywa na
jarida moja lijulikanalo kama Journal of Agriculture and Food Chemistry,
unaonesha kuwa mbali ya maharage kuwa na kiwango kikubwa cha faiba, pia
maharage yana virutubisho vingine vinavyojulikana kama Anthocyanins ambavyo
hutoa kinga mwilini Antioxidant. Kiwango cha virutubisho hivyo kilichomo kwenye
maharage, kinaelezwa kuwa ni kikubwa kuliko hata kinachopatikana kwenye matunda
kama zabibu ambayo inaaminika kuwa na kiwango kikubwa zaidi.
Pia watafiti walipofanya tathmini ya ziada
kwenye maharage, waliweza kubaini kuwa maharage yanapokuwa meusi zaidi, ndivyo
ambavyo kiwango kikubwa cha kinga kinavyoweza kupatikana, yakifuatiwa na
maharage ya rangi nyekundu, kahawia, njano na mwisho meupe. Hii ina maana
kwamba maharage meusi ndiyo yana virutubisho vingi zaidi kuliko maharage meupe na rangi nyingine.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv