MIONGONI ya masuala muhimu, mzazi unapaswa kuyazingatia katika malezi ya mtoto wako. Ikiwa mambo hayo yatasimamiwa vizuri ni wazi mtoto wako atapiga hatua vizuri katika ukuaji wake na hata kufikia kuwa mtoto mwema.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Parenting. Com, mzazi ana mchango mkubwa katika ukuaji wa mtoto wake. Kwa kuwa kila mtoto ana hatua katika ukuaji, mtoto mdogo mwenye umri mdogo huhitaji usaidizi ili aweze kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Ili mwanao aweze kutoka hatua moja kwenda nyingine, kama mzazi au mlezi unahitaji kumchochea na kumhamasisha kufanya vitu fulani fulani. Najua una hamu ya kufahamu ni kwa vipi unaweza kumchochea mwanao hata kumudu kufanya yale asiyoweza.
Kama ulikuwa hujaanza bado hujachelewa. Hii ni njia itakayomsaidia mwanao kujifunza kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Zifuatazo ni dondoo hizo:
Kucheza
Kitendo cha kucheza naye mpira, kutamsaidia kuwa makini. Unampigia taratibu atakuwa na hamu ya kupiga na yeye. Hivyo wakati mkiendelea na mchezo, atazidi kuongeza ari ya uchezaji.
Pia kama alikuwa anakosea utamuona anajirejkebisha taratibu. Kwa kuwa michezo ni njia moja wapo ya kumfanya achangamshe akili yake na pia kukuza uwezo wake wa kufikiri.
Kuongea
Imezoeleka kwa watu wengi kupenda kuongea na watoto kitoto. Kama mzazi unatakiwa uongee naye kama vile unaongea na mkubwa. Hii itamsaidia kujifunza misamiati mipya.
Kwa kawaida mtoto hujifunza kuongea kupitia mzazi wake. Pia hili hutokea katika kipindi hiki cha utoto. Hivyo ni vyema kulifahamu hili kwa uzuri kwa faida ya mtoto wako.
Kwa kuwa mtoto ni kama karatasi isiyoandikwa inakuwa rahisi kwake kuandika kitu kikonekana kwa urahisi. Vivyohivyo katika hili, unapoongea na mtoto wako maneo yanayeleweka kama unavyofanya kwa mtu mzima inakuwa ni rahisi kwake kujifunza kuongea na kujua lugha kwa urahisi.
Kutembea
Mhamasishe kuanza kutembea kwa kumuacha ajishikilie kwenye kitanda, meza au kwenye samani nyingine. Muwekee mdoli wake anaoupenda kwa mbali na kisha mwache afuate. Mwanzo ataanza kujivuta baadaye taratibu ataanza kupiga hatua akifuata.
Ikiwa ataonyesha kuchoka kusimama, usimlazimishe, mwache apumzike. Atakapoanza kujaribu kunyanyuka na kuinua miguu mwenyewe mwache afanye hivyo isipokuwa hakikisha unamfurahia anapoweza, unaweza kumshangilia kwa kumpigia makofi hii itamuhamasisha.
Kula
Katika umri huu mdogo, unaweza sio tu kumfundisha mwanao kula, bali kumhimiza kula bila kumlazimisha. Unapotaka kumpa chakula hakikisha unaongea naye ili ahamasike na kula kwa urahisi.
Mhamasishe mwanao kula mwenyewe kwa kumuweka kwenye mkeka au mezani na kumpa chakula na mwache ale mwenyewe. Ulaji huu uwe wa vyakula bora kwani kwa kumpa chakula bora mwanao utamwondoa kwenye hatari ya kupata matatizo kiafya.
Vitu kama pipi, biskuti wakati mwngine ni chanzo cha kuharibu meno ya mwanao. Hivyo kama mzazi unatakiwa kuelewa vyakula vitakavyompa mwanao afya bora na siyo vinginevyo. Mzoeshe kula machungwa, embe na hata nanasi kwani ni bora zaidi kuliko soda au juisi ya kopo.
Moto au baridi
Anza kumfundisha dhana ya moto na baridi. Taratibu mgusishe chapati ya moto na sema “ya moto” kisha mgusishe glass ya baridi na kisha mwambie “ baridi
source #mwananchi
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv