HII ni hatua ya kwanza kwa mtoto ndio nyingine zinafata kama  kutambaa,kusimama na kutembea, wazazi wengi wanasubiri hii hatua hii ya kukaa.

Mtoto anapofikisha miezi 3 shingo yake inakuwa imeshakaza ingawa kuna wengine shingo zinachelewa kukaza ukuaji wa watoto unatofautiana mzazi usije ukapanic ukiona mtoto kachelewa.Kwenye ukuaji wa watoto ni zoezi linalochukua mda mzazi hutakiwi kumfunza mapema mtoto kukaa au kutembea kabla ya mda wake.

Hizi hapa ni Dalili za mtoto anaetaka kujifunza kukaa 
Utakapo mlazimisha mtoto kukaa kabla ya mda wake utamuumiza mgongo au hata kumtegua uti wamgongo.Hakikisha mtoto wako misuli, zake zimekaza  za shingo misuli ya tumbo,mgongo,miguu na mabega nayo iwe imeshakaza na ukimbeba utamwona anataka kukaa mwenyewe iyo nayo ni ishara kubwa.

Kukaa kwa mtoto kunaanza akiwa na miezi 4-7 kuna wanaowahi kukaa au wakuchelewa kukaa ,unatakiwa umpe support akiwa anataka kukaa unaweza mwekea mto kwenye kona ya sofa ukamkalisha lazima uwe pembeni yake ili asianguke , mkalisha chini ukamshika mgongo wake kwanyuma kumpa support tumia dakika 5-10 kwa siku ukiwa unamfunza kukaa.

Hakikisha anakuwa na toys za kuchezea,ukiwa unamchezesha mwonyesha toys na itamfanya kunyoosha shingo kuziangalia inamsaidia kukaza misuli ya shingo kipindi amekaa au amelalia tumbo (tummy),mnunulie toys za rangi rangi na zenye milio tofauti unaponunua hakikisha unanunua ya kulingana na umri wake ,usimnunulie za watoto wakubwa zikamuumiza pindi achezeapo.

Kwenye kumfunza mtoto kukaa  mzazi unakaa chini tanua miguu yako mkalishe chini mtoto katikati ya mapaja yako kiasi cha kwamba akianguanguka ataangukia kwako kwa usalama zaidi,kuna viti vya kumfunza mtoto kukaa vinaitwa bumbo floor seat ila utakapo mkalisha mweke sehemu flat sakafuni hakikisha umemfunga mikanda pindi akaliapo hiko kiti.

MWISHO. Kuwa makini sehemu utakayo mweka kulalia tumbo au kuajifunza kukaa isiwe kitandani au juu ya meza,iwapo utamlaza/ mkalisha kitandani hakikisha uponae karibu  ili asianguke, na kama ni chini kuwe kusafi kusiwe na vitu vya yeye kuokota na kuweka mdomoni.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz_blog  , inst@edonetz_blog na  youtube@edone tv
 
Top