JINSI YA KUMFURAISHA MUMEO KILA SIKU.
1- Mapokezi mazuri
a) Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.
b) Mpokee kwa uso mchangamfu
c) Jipambe na ujitie manukato (Perfume)
d) Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote mbaya mpaka atapokwisha pumzika
e) Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shauku
f) Fanya jitihada kubwa katika mapishi mazuri na kitayarishe kwa wakati.
2- Ipambe na ilainishe sauti
a) Ni kwa ajili ya mumeo peke yake, isitumike mbele ya wanaume wasio mahram (wanaume wanaoweza kukuoa iwapo utakuwa huna mume)
3- Harufu nzuri na kujipamba mwili
a) Ushughulikie vyema mwili wako na afya yako.
b) Vaa nguo za kuvutia na jitie manukato.
c) Koga mara kwa mara, na baada ya siku za hedhi, safisha madoa madoa yote ya damu na ondosha harufu mbaya.
d) Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.
e) Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa, mfano wa tattoo.(kuchorwa mwili kwa kitu cha moto kwa ajili ya pambo.)
f) Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.
g) Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara.
h) Hata hivyo usifanye israfu katika vitu hivi, na bila shaka fanya hivyo mbele ya mahram zako na wanawake wenzako tu.
4- Jimai (Tendo la ndoa)
a) Harakisha kufanya jimai pale mumeo anapokuwa na hamu ya tendo hilo.
b) Weka mwili wako safi na wenye kunukia kadri iwezekanavyo pamoja na kujisafisha maji maji yanayotoka wakati wa jimai.
c) Semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo.
d) Mwachie mumeo atosheleze kabisa hamu yake.
e) Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya jimai, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.
5- Kutosheka na kile ulichojaaliwa
a) Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au na aina ya kazi anayofanya.
b) Uwaangalie masikini, wagonjwa, na vilema na kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa yote yale uliyopewa.
c) Ni lazima ukumbuke kuwa utajiri wa kweli upo katika Iman na uchaji Allaah.
6- Kutoshughulishwa na mambo ya kidunia
a) Usiichukulie dunia hii kuwa ya matumaini na kushughulishwa nayo.
b) Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima.
c) Kutosheka na kuishi maisha ya kawaida hakuna maana ya kutofurahia/kutotumia kilicho kizuri na kilichoruhusiwa (halali), bali kunamaanisha mtu kuangalia akhera yake na kutumia kile ambacho Allaah Amempa kwa ajili ya kupata Pepo (Jannah).
d) Muhimize mumeo kupunguza matumizi na kubakisha fedha kwa ajili ya kutoa sadaka na kuwalisha masikini na wasiojiweza
7- Shukurani
a) Kutokana na hadithi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wengi wa watu wa motoni ni wanawake kwa sababu hawana shukurani na kutoridhia wema wanaofanyiwa.
b) Matokeo ya kuwa na shukurani ni kuwa mumeo atakupenda zaidi na atafanya awezalo kukufurahisha kwa njia nyingi.
c) Matokeo ya kutokuwa na shukurani ni kuwa mumeo atavunjika moyo na ataanza kujiuliza: Kwa nini nilazimike kumfanyia wema hali ya kuwa hana shukurani?
8- Kujitolea na Twaa
a) Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano ajali au kufilisika.
b) Kumpa msaada kwa kufanya kazi, msaada wa fedha, na vitu vyengine iwapo utahitajika.
9- Kumtii
a) Kumtii katika yote anayokuamrisha, isipokuwa katika yale yaliyoharamishwa.
b) Katika Uislam, mume ndie kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.
10- Kumliwaza anapokasirika
a) Kwanza kabisa, jaribu kujiepusha na kile ambacho una uhakika kuwa kitamkasirisha.
b) Bali iwapo imetokezea kuwa huwezi, basi jaribu kuepusha ugomvi kwa njia zifuatazo:
1. Iwapo wewe ndiye uliyekosea, basi mtake radhi (muombe msamaha)
2. Iwapo yeye ndiye aliyekosea basi:
- Endelea kunyamaza badala ya kubishana au
- Samehe haki yako au
- Subiri hadi zitakapokwisha hasira zake na mlijadili suala hilo kwa amani
3. Iwapo amekasirishwa na mambo nje ya nyumba basi:
- Endelea kunyamaza kimya hadi hasira zake zitapokwisha
- Mpe udhuru (wa hasira zake), mfano kuchoka, matatizo kazini, kuna mtu amemuudhi.
- Usimuulize masuala mengi na kushikilia kujua nini kimetokezea, mfano (kumwambia) (1) Ni lazima unieleze nini kimetokezea. (2) Ni lazima nijue nini kimekukasirisha namna hiyo. (3) Unanificha kitu, na mimi nina haki ya kujua.
11- Muongozo (na majukumu) anapokuwa hayupo:
a) Jilinde na mahusiano yoyote yaliyokatazwa.
b) Zidhibiti siri za familia, hususan jimai (tendo la ndoa) na mambo ambayo mumeo hapendi watu wengine wayajue.
c) Ishughulikie nyumba na watoto.
d) Ishughulikie mali yake na vitu vyake.
e) Usitoke nje ya nyumba yako bila ya ruhusa yake na bila ya hijaab iliyo kamili.
f) Usikaribishe watu ambao mumeo hapendi kuja kwao.
g) Usimruhusu mwanamme yeyote asie Mahram wako kuwa nawe faragha pahala popote.
h) Kuwa mwema kwa wazazi wake na jamaa zake akiwa hayupo.
12- Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake
a) Ni lazima uwakaribishe wageni wake na ujaribu kuwafurahisha, hususan wazazi wake.
b) Ni lazima uepuke matatizo kati yako na jamaa zake kwa kadri iwezekanavyo.
c) Ni lazima uepuke kumuweka pahala ambapo inambidi achague kati ya mama yake na mkewe.
d) Onyesha urafiki (makaribisho mazuri) kwa wageni wake kwa kuwatayarishia pahala pazuri pa kuketi, chakula kizuri, kuwakaribisha vizuri wake zao, n.k.
e) Muhimize kuwatembelea jamaa zake na uwaalike nyumbani kwako.
f) Wapigie simu wazazi na dada zake, watumie barua, na wanunulie zawadi, wasaidie wakati wanapoharibikiwa, n.k.
13- Wivu wenye kukubalika
a) Wivu ni aina ya mapenzi ya mke kwa mumewe bali ni lazima ubakie katika mipaka ya Uislam, mfano kutowatukana na kuwasengenya wengine, kuwavunjia heshima zao, n.k.
b) Usifuate au kuanzisha tuhuma zisizo na msingi
14- Subira na kumpa moyo
a) Kuwa na subira mnapokabiliwa na umasikini na hali ngumu (kimaisha na kifamilia).
b) Wakati mnapokabiliwa na majanga na maharibiko ambayo yanaweza kutokea kwako, kwa mumeo, kwa watoto wako, jamaa au mali, mfano magonjwa, ajali, kifo, n.k.
c) Wakati mnapokabiliwa na matatizo katika Da’wah (kufungwa jela, kukamatwa, n.k.), kuwa na subira na mhimize katika kubaki katika njia ya Allaah na kumkumbusha kuhusu Pepo.
d) Anapokufanyia uovu, mlipe uovu wake kwa kumfanyia wema.
15- Msaidie katika kumtii Allaah, Da'awah (Ulinganiaji) na Jihaad
a) Shirikiana na mumeo na mkumbushe ibada mbali mbali za faradhi na za Sunnah.
b) Muhimize kusali usiku.
c) Sikiliza na soma Qur-aan peke yako na ukiwa pamoja na mumeo.
d) Mkumbuke (mtaje) Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) sana, hasa hasa baada ya Alfajiri na kabla ya Magharibi.
e) Pangeni pamoja shughuli za Da’wah kwa wanawake na watoto.
f) Jifunze hukumu za Kiislam na adabu za Kiislam kwa wanawake.
g) Msaidie mumeo katika shughuli zake kwa kumhimiza, kumpa ushauri mwema, kumliwaza machungu yake, n.k.
h) Samehe baadhi ya haki zako na samehe sehemu ya muda wako wa kuwa pamoja na mumeo kwa ajili ya Da’wah.
i) Mhimize kwenda Jihad anapohitajika na mkumbushe kuwa wewe na watoto mtakuwa katika hifadhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).
16. Utunzaji mzuri wa Nyumba
a) Iweke nyumba safi, weka mapambo na iweke katika mpangilio mzuri.
b) Badilisha mpangilio wa nyumba mara kwa mara ili kuzuia kupoteza hamu nayo na kuchoshwa nayo.
c) Tayarisha chakula kizuri na chenye afya.
d) Jifunze ujuzi wowote wa muhimu kuhusu uangalizi wa nyumba, mfano kushona, n.k.
e) Jifunze namna ya kuwalea vyema watoto na kwa njia ya Kiislam.
17- Kuhifadhi/Kutunza fedha na familia
a) Usitumie fedha zake, hata kwa sadaka bila ya ruhusa yake labda uwe na uhakika kuwa atakubaliana na matumizi hayo.
b) Ilinde nyumba yake, gari, n.k. anapokuwa hayupo.
c) Waweke watoto katika hali nzuri, nguo safi, n.k. Zingatia lishe yao, afya, elimu, tabia, n.k wafunze Uislam na wahadithie visa vya Mitume ('Alayhimus Salaam) na Maswahaba (Radhiya Allaahu 'anhum).
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv