Image result for PUSH UP
karibu leo, tuangazie moja ya mazoezi yenye matokeo mazuri kwa viungo vya binadamu tena bila ya kutumia kifaa chochote. Ambayo ni  Push up. Push up ni moja ya mazoezi yanayojenga afya njema kwani push up zinasaidia kuimarisha kifua, mabega misuli ya mikono.
Image result for PUSH UP
Jinsi ya kufanya push up: Uso wako ukiwa unatizama chini, weka mikono yako kwenye sakafu, itanue izidi kidogo mabega yako (kama inavyoonekana kwenye picha).

Hakikisha vidole vyako vya miguu vipo sakafuni, kama hii ni ngumu, basi unaweza kuanza kwa kuweka magoti yako chini.

Hakikisha mwili wako umenyooka kuanzia vidoleni hani kichwani.

Kunja mabega yako mpaka uwe kama unagusa sakafu.

Rudi juu kwa kujinyanyua kwa kutumia mabega, hakikisha mwili wako umenyooka mwanzo hadi mwisho.

Fanya hivi mara kadhaa ukiwa unaongeza idadi siku hadi siku.

Hauna haja ya Gym, hauna haja ya kununua kifaa chochote, unaweza kufanya zoezi hili hata ukiwa ofisini. Na hii ndio dondoo ya leo.
 JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top